Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akizungumza na
Watendaji wa Chama na Makatibu wa siasa na uenezi kuanzia ngazi za
matawi, wadi, hadi makatibu wa siasa na uenezi kuanzia ngazi ya Tawi
hadi jimbo, wakati akifungua Mafunzo elekezi ya siku moja yaliyofanyika
katika hoteli ya Villa iliyopo Maruhubi.
Na Is-haka Omar, Zanzibar.
NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Nd. Vuai Ali Vuai amewasihi Viongozi wa
ngazi mbali mbali za Chama kuendeleza utamaduni wa kuandaa mafunzo
ya kuwajengea uwezo Watendaji wao ili wawe na uelewa na ujuzi wa
kutekeleza shughuli za Chama kwa ufanisi.
Akizungumza
katika Ufunguzi wa Mafunzo elekezi ya Watendaji wa Chama na Makatibu
wa Siasa na Uenezi kuanzia ngazi za Matawi, Wadi hadi Jimbo Wilaya ya
Amani Kichama yaliyofanyika katika Hoteli ya Villa iliyopo Maruhubi
Nje Kidogo ya Mjini wa Zanzibar.
Alisema
mafunzo ni nyenzo muhimu inayosaidia kuwaongezea maarifa na mbinu
mbadala za kiutendaji watumishi na watendaji wa taasisi ili wafanye
kazi zao kwa kujiamini zaidi.
Vuai
Alifafanua kuwa CCM inakabiliwa na majukumu ya Uchaguzi wa Chama na
Uchaguzi Mkuu wa Dola hivyo watendaji wa chama hicho wanatakiwa
wanatakiwa kuandaliwa vizuri kupitia mafunzo ya chama kwa lengo la
kukumbushwa baadhi ya majukumu yao ya msingi yakiwemo matumizi sahihi ya
kanuni, katiba na miongozi ya Chama kwa makada wengine.
“Tuendelee
kufanya mafunzo kwa wingi kadri hali itakavyoruhusu kwani ni jambo
muhimu kwa binadamu yeyote yule anayetaka maendeleo mazuri ya kazi yake
kwa lengo la kuongeza ujuzi na ufanisi katika utekelezaji wa
shughuli zetu za kisiasa ndani na nje ya Chama chetu.”, alisema Vuai na
kuongeza kuwa mafunzo yatawasaidia watendaji hao kuelewa kwa upana
wanayoyafanya na kuepuka athari ya kufanya kazi kwa mazoea.
Naibu
Vuai alieleza kwamba utaratibu wa mafunzo umeanza zamani ambapo Chama
kilikuwa na vyuo vyake maalum vya kuwaandaa makada , watendaji na
viongozi makini waliokuwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja na
kuzisimamia katika kuimarisha maendeleo ya Chama.
Alisema
kwa mujibu wa ibara ya 5 ya Katiba ya Chama hicho ni kushika Dola
Tanzania bara na Zanzibar serikali za mitaa na serikali kuu, hivyo
amewapongeza makada hao kwa uwezo na jitihada zao za kuahakikisha kila
uchaguzi toka umeanza mfumo wa vyama vingi CCM imekuwa ikishinda.
Aidha
aliwataka watendaji hao kuanzia ngazi za Matawi hadi Wilaya kutumia
fursa walizokuwa nazo katika maeneo yao kwa kuanzisha miradi mbali mbali
itakayowasaidia kupata kipato cha kutatua baadhi ya changamoto
zinazohitaji fedha na kujitegemea wenyewe badala ya kuendelea
kuwategemea Viongozi wa majimbo pekee.
Hata
hivyo aliendelea kuwakumbusha washiriki wa mafunzo hayo kwamba
Watendaji watakaopata fursa ya kugawa fomu za kugombea Uongozi ndani ya
CCM waongeze bidii katika kutenda haki kwa kuhakikisha kila mwanachama
mwenye sifa ya kuchagua na kuchaguliwa anapata haki hiyo kwa mujibu wa
ibara ya 14 ya Katiba ya Chama hicho.
“
Najua watendaji na viongozi wa CCM ni waadilifu lakini naomba tuongeze
umakini katika suala la Uchaguzi wa Chama kwa kuwapatia fomu wale wote
wenye Haki ya kuchagua na kuchaguliwa msiwanyime fursa hiyo kama mtu
hafai basi mwacheni akanyimwe kura na wanachama wenzake lakini nyinyi
msihusike na kufanya hivyo kutapunguza malalamiko .”, alisisitiza
Vuai.
Naye
Katibu wa Wilaya ya Amani Kichama, Abdallah Mwingi amesema lengo la
mafunzo hayo kwa lengo la kuzidi kuwajengea uwezo watendaji hao ili
waweze kusimamia ipasavyo Chaguzi za Chama na Dola zijazo kwa kuwachuja
wanachama wanaotaka nafasi za uongozi na kuwapata viongozi ambao ni
waumini wa dhati wa itikadi na sera za CCM na serikali zilizopo
madarakani.
Alisema
Wilaya hiyo imekuwa ikifanya kazi ya ziada ya kuimarisha chama kwa
kuongeza wanachama wapya na kuwapatia mafunzo maalum kupitia madarasa
ya itikadi kwa lengo la kuwajenga kuwa waumini wa kweli watakaosimamia
maslahi ya CCM bila ya hofu.
Akitoa
maneno ya Shukrani Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Salim Hassan Turky,
amesema washiriki hao watazifanyia kazi nasaha hizo kwa lengo la
kuhakikisha CCM inaendelea kuwa Chama bora kinachokubalika kwa wananchi.
Aliwasihi
watendaji hao makundi ya kukigawa chama wakati wa Uchaguzi kwani
kuna baadhi ya watendaji waliowahi kusimamia chaguzi zilizopita wamekuwa
wakilalamikiwa kwa kufanya upendeleo kwa baadhi ya Wagombea wanaowataka
na hatimaye wanapatikana viongozi wenye sifa za kutilia shaka.
Aliwaomba
washiriki hao kuwasaidia na kuwaongoza wanachama wa Chama hicho
katika kuanzisha miradi midogo midogo kuanzia ngazi za Mashina hadi
Mikoa, itakayoweza kuwasaidia kujiajiri wenyewe na kukuza Uchumi wa
nchi.
0 comments:
Post a Comment