Tunapenda
kuwafahamisha wanachama wa ACT Wazalendo na umma wa watanzania kwa
ujumla, kuwa kampeni kwa ajili ya chama cha ACT Wazalendo katika jimbo
la Dimani visiwani Zanzibar na kata mbali mbali kwa Tanzania bara ambazo
chama kimesimamisha wagombea zitafunguliwa rasmi disemba 31/2016
Kwa
upande wa udiwani chama kilisimamisha wagombea saba na waliopitishwa na
Tume ya uchaguzi ni wagombea sita baada ya mgombea wa kata ya
Misugusugu mkoani Pwani kuenguliwa kugombea kutokana na pingamizi
alilowekewa
Kata
ambazo chama cha ACT Wazalendo imesimamisha wagombea ni pamoja na
Isagahe,iliyopo Kahama mkoani Shinyanga,Kijichi, iliyopo Temeke jijini
Dar esSalaam,Nkome iliyopo Mkoani Geita,Tanga iliyopo mkoani Ruvuma na
Ihumwa iliyopo mkoani Dodoma.
Chama
cha ACT wazalendo kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika
maeneo tuliyosimamisha wagombea wetu na kuleta mabadiliko ya kiutendaji
na kiuawajibikaji katika maeneo hayo huku tukitanguliza uzalendo kwa
Taifa letu.
Pale
ambapo chama hakijasimamisha mgombea, wanachama, wafuasi na wapenda
demokrasia na mabadiliko ya kweli tunawaomba wahakikishe wanamchagua
mgombea wa upinzani ambaye ana nguvu katika eneo hilo
Tunawahimiza
wanachama wetu na wapenzi wa demokrasia popote pale walipo katika kata
zinazofanyika uchaguzi kuhakikisha wanaiondoa CCM kwa kuwachagua
wagombea wa vyama vya upinzani kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao
Imetolewa na Abdallah Khamis
Afisa Habari ACT Wazalendo
27/12/2016
0 comments:
Post a Comment