Na Is-haka Omar, Zanzibar.
NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema Chama hicho
kitaendelea na utamaduni wa kutoa mafunzo kwa watumishi na watendaji
wake ili waweze kufanya kazi kwa mujibu wa matakwa ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020.
Aliyasema
hayo katika hafla ya kuwakabidhi vyeti watendaji wa Chama Unguja na
Pemba huko katika Ukumbi wa Makao makuu ya Chama Cha CCM Kiswandui
Zanzibar.
Alisema
anamamini elimu waliyoipata matendaji hao itaweza kuwasaidia kuongeza
uwezo na ufanisi katika shughuli zao za kiutendaji katika ofisi zao kwa
wageni wanaofika katika maofisi yao.
Vuai alieleza mafunzo
hayo yametokana na matakwa ya ibara ya 188 ya Ilani ya uchaguzi ya CCM
ya mwaka 2015/2020 inayoelekeza kutolewa kwa mafunzo zaidi kwa makada na
viongozi mbali mbali ili wawe na weledi mkubwa katika masuala tofauti
ya Chama.
Alisema
licha ya ilani ya ccm kuagiza kufufua vyuo vya uongozi na siasa vya CCM
ambavyo ni ilemi na Tunguu huku wakifikiria maamuzi ya kuendesha mafunzo
ya kuwajengea uwezo watendaji hao kadri uwezo wa uendeshaji wa mafunzo
utakavyoruhusu.
“
Tumieni mafunzo haya kama fursa ya kujiongeza kiutendaji ili muweze
kufanya kazi zenu kwa weledi na kujiamini zaidi.”, alisema Vuai.
Hata
hivyo aliahidi kuwa mafunzo hayo yatafanyika kwa awamu mbali mbali
kadri uwezo wa uendeshaji wake utakavyoruhusu ili Watumishi na watendaji
waweze kupata fursa hiyo ya kitaaluma.
Alifafanua kuwa taaluma waliyopata itawasaidia katika majukumu mbali mbali yakiwemo uchaguzi
katika chama na kuwataka ifikapo mwakani watoe fomu ya uongozi kwa kila
mwanachama aliyekuwa na sifa na bila ya upendeleo ili zoezi hilo
likfanikiwe kwa asilimia kubwa.
Nae mshiriki wa
mafunzo mafunzo hayo katibu wa CCM wilaya ya Mkoani Pemba Abdalla
Yussuf Ali alisema mafunzo hayo watafanyia kazi kama ilivyokusudiwa
sambamba na kuitumia elimu waliyoipata.
Aidha alisema kuwa wataitumia elimu hiyo kwa kwa kuleta tija ya kuonekanwa kuwa ofisi zao zitakuwa ni za mfano na za kuigwa.
Mafunzo hayo ya mwezi mmoja ziliwasilishwa
mada sita ambazo ni Uanzishwaji masjala na utunzaji kumbukumbu za Ofisi
kwa usalama, Uendeshaji wa shughuli za Ofisi na mawasiliano ya kiofisi
na Taratibu za uendeshaji wa mikutano.
Zingine ni Dhana
ya utawala bora na uzalendo katika utandawazi pamoja na Huduma kwa
mteja na utunzaji wa muda, yalikuwa na washiriki 42 kutoka Pemba na
Unguja.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment