Na. Aron Msigwa –NEC.
25/1/2017.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa Kura 234 ziliharibika katika Uchaguzi mdogo
wa Ubunge katika jimbo la Dimani, Zanzibar Januari 22, 2017.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) Bw. Ramadhan Kailima amesema kuwa Wapiga Kura walioandikishwa katika
jimbo la Dimani, Zanzibar ni 9,275.
Amesema kati ya hao wapiga Kura 6,406 walijitokeza
kupiga Kura siku hiyo ambapo Kura halali zilikuwa 6,172 na Kura zilizoharibika
zilikuwa 234.
“Napenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa taarifa
sahihi za matokeo ya Kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani ni
kama ifuatavyo; Wapiga Kura walioandikishwa jimbo la Dimani ni 9,275, Waliopiga
Kura walikuwa 6,406, Kura halali 6,172 na Kura zilizoharibika ni 234”
Amesisitiza.
Mkurugenzi Kailima ameeleza kuwa katika Uchaguzi huo
vyama 11 vilikuwa na wagombea wa Ubunge ambapo Chama cha ACT-Wazalendo kilipata
Kura 8, Chama cha ADC Kura 42, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kura 4860, CHAUMA Kura
10, Chama Cha Wananchi CUF Kura 1234, Chama cha DP Kura 8.
Vingine ni Chama cha NRA kura 1, SAU Kura 4, TLP kura
2, Chama Cha UMD Kura 2 na Chama Cha UPDP Kura 1 na kufanya jumla ya Kura za
Vyama vyote kuwa 6172.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment