NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
CHAMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema dhana ya kuanzishwa kwa
fikra ya Umoja wa kitaifa ilianzia kwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa
Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume, na sio ajenda ya vyama vya
upinzani.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar Dkt.
Abdallah Juma Abdallah “Mabod” wakati akizungumzia historia ya maisha
ya Mwasisi wa ASP ambayo ni CCM kwa sasa Marehemu Mzee Karume huko
Afisini kwake Kisiwandui Unguja.
Amesema
Mwasisi huyo alikuwa ni kiongozi anayepinga utengano na ubaguzi misingi
ya kidini, kikabila na kisiasa ndio maana katika Baraza la mwanzo la
Mawaziri kupitia Baraza la Wawakilishi la Wakati huo aliteuwa baadhi ya
viongozi wa vyama vya upinzani ili kujenga Umoja wa kitaifa na kuondosha
ubaguzi.
Aidha
alisema kuwa viongozi walioteuliwa kutoka vyama vya upinzani walikuwa
ni waadilifu waliofuata miongozo na matakwa ya serikali kwa wakati huo
licha ya kujitokeza kwa vitendo vya usaliti kwa viongozi hao.
“
Mzee karume alikuwa na moyo wa huruma na akiwapenda wananchi wa visiwa
vya Zanzibar wawe na maendeleo endelevu.”, alisema Dkt. Mabodi.
Naibu
Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa lengo la kufanyika kwa Mapinduzi ya
Mwaka 1964, lilikuwa ni kurejesha heshima ya wazawa waliotawaliwa
kimabavu na utawala wa Kisultani kwa zaidi ya miaka 100.
Alisema
baada ya mapinduzi hayo Marehemu Mzee Karume na Jopo lake la Umoja wa
Vijana wa ASP, waliweka mipango mikakati ya kuimarisha maendeleo ya
Zanzibar.
Pia
aliweka vipaumbe mbali mbali vikiwemo kuanziasha mpango wa kuboresha
Sekta ya Elimu na Afya kwa kuwapeleka vijana mbali mbali nje ya nchi
ikiwemo China, Urusi, Cuba na mataifa mengine ili wapate utalamu wa fani
tofauti zikiwemo Udaktari na masuala ya Uongozi ili kuharakisha
maendeleo ya nchi.
Hata
hivyo aliweka mfumo wa Elimu bure ili Watoto wa Kiafrika waliokuwa
hawana fursa ya kusoma wakati huo wajifunze na kuelimika ili waweze
kusaidia katika masuala mbali mbali ya kiutendaji.
Dkt.
Mabodi alisema kuwa Mzee Karume alikuwa ni kiongozi jasiri na asiyetaka
kukaa Ofisini bali alikuwa akitembea maeneo mbali mbali na kujionea
mwenyewe changamoto zinazowakabili wananchi, tofauti na baadhi ya
viongozi wa sasa wanaosubiri taarifa za utekelezaji ofisini.
Hata
hivyo alisema Mzee Abeid Amani katika Harakati za kupinga ubaguzi ambao
ulikuwa umejenga ngome, enzi za utawala wa kifalme aliwatangazia
wananchi kuwa wanatakiwa kuoana makabila mbali mbali ili kuchanganya
rangi kwa lengo la kufuta ubaguzi uliokuwa kukisambazwa na watu
waliokuwa ni miongoni mwa Waliopinduliwa.
Aidha
alisema Mzee Karume pamoja na mambo mema aliyoyafanya enzi za uhai wake
pia ni mwasisi wa kwanza wa Demokrasia kwani aliwakaribisha mataifa
mbali mbali kuja Zanzibar kuwekeza na kushauri masuala ya Kisiasa.
Aliimarisha
miundombinu ya barabara na kujenga nyumba za kisasa ambazo hivi sasa
zinajulikana kama nyumba za maendeleo Unguja na Pemba.
Pia
aliimarisha Sekta ya Mawasiliano kwa kuanzisha Televisheni ya mwanzo ya
rangi Afrika Mashariki na kati iliyoitwa TVZ ambayo kwa sasa ni ZBC TV,
sambamba na radio ya kisasa ya Sauti ya Tanzania Zanzibar.
Naibu
Katibu Mkuu huyo aliweka wazi kuwa kiongozi huyo ametenda mengi mazuri
kwa nchi ya Zanzibar, hivyo viongozi na watendaji wa sasa waendeleze
mambo mema yaliyoachwa huku nao wakibuni vitu vingine vipya
vinavyoendana na wakati uliopo sasa.
Pia
alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt.
Ali Mohamed Shein kwa kufanyia kazi kwa vitendo kauli mbiu ya “ Zanzibar
kujitawala yenyewe kielimu, kiafya na kimiundombinu ya kisasa” huku
ikipiga vita adui ujinga na maradhi.
Pamoja
na hayo alimpongeza pia Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa msimamo wake wa kulinda Muungano wa Serikali
mbili na Mapinduzi ya Zanzibar mambo ambyo ndio urithi wa Waasisi wa ASP
na TANU wakiwemo Marehemu Mzee Karume na Hayati Mwl. Nyerere.
Pamoja
na hayo aliwambia wananchi kuwa kila ifikapo April 7 ya kila mwaka ni
maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya mashujaa wa Zanzibar na waasisi
wote waliofariki , na sio sherehe ndio maana panafanyika hitima na
kuombwa dua kwa lengo la kuenzi juhudi zao.
0 comments:
Post a Comment