NA IS-HAKA OMAR, PEMBA.
BAADHI
ya wananchi kisiwani Pemba wameshauriwa kuacha siasa za visasi na
chuki zinazochangia kuongezeka vitendo vya uhalifu wa mali na kuharibu
heshima ya nchi kitaifa na kimataifa.
Ushauri
huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma
Saadala katika mwendelezo wa ziara zake za kuimarisha uhai wa chama huko
Tawi la CCM Kengeja, Mkoa kusini Pemba.
Alifafanua
kwamba hali hiyo sio kwamba inaishia kuathiri uchumi na siasa za nchi
peke yake bali vinaenda mbali kwa kuathiri maisha na undugu wa damu
uliopo hata kabla ya kuanzishwa kwa mifumo ya kisiasa nchini.
Nasaha
hizo alizitoa baada ya kuwepo kwa malalamiko ya uharibifu wa
miundombinu ya maji safi na salama katika shehia hiyo, iliyoharibiwa na
baadhi ya watu kwa kujenga zenge la kuzua maji yasiwafikie wananchi wa
eneo hilo.
“
Serikali inarahisha huduma kwa wananchi kwa kuwajengea miundombinu
rafiki ya upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma nyingine
muhimu lakini baadhi yenu wanaharibu kwa makusudi kutokana na masuala ya
UCCM na UCUF, hilo sio sahihi kabisa lazima tubadilike kwa kuacha tabia
hizo.”, alisema Dkt. Mabodi.
Hata
hivyo alitoa wito kwa vyombo vya Dola kutoa taarifa na ripoti za
kudhibiti vitendo hivyo kwa vyombo vya habari ili jamii ijue utekelezaji
wake.
Aliwambia
wanachama wa chama hicho kwamba waendelee kushikamana na kuwa
watulivu na wasilipize visasi na badala yake waendelee kutenda wema na
kuwaelimisha watu waohusika na hujuma hizo ili waweze kubadilika na
kujiunga na chama hicho.
Aliwataka
baadhi ya vijana wanashutumiwa kujihusisha na vitendo hivyo kuacha, na
kutafakari kwa kina athari zake kwani zinawaumiza Watu wenye ulemavu,
Wazee pamoja na wagonjwa waliopo hospitalini wanaohitaji huduma hizo
wakati wote.
Pamoja
na hayo alisisitiza umuhimu wa wanachama kushiriki katika zoezi la
uchaguzi wa ndani ya chama na Jumuiya katika zoezi linaloendelea hivi
sasa ili wapatikane viongozi wenye uwezo wa kukiletea chama ushindi wa
ngazi zote za uchaguzi mwaka 2020.
Wakati
huo huo, Naibu Katibu Mkuu huyo alipongeza Mwakilishi wa Jimbo la Ole,
Mussa Ali Mussa kwa juhudi zake katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi wote licha ya kukabiliwa na
vikwazo vya kisiasa kutoka kwa wapinzani.
Akitoa
tathimini ya masuala ya ulinzi na usalama Mkuu wa Wilaya ya Chake
Chake, Salama Mbarouk Khatib alisema toka kumeanzishwa doria za mara kwa
mara ndani ya eneo hilo vitendo vya uhujumu mali na miundombinu ya umma
vimepungua.
Hata
hivyo alisema na kutoa onyo kali kwa baadhi ya wananchi wanaoendelea na
tabia ya kufunga Ng’ombe katika mifereji ya maji safi na kusababisha
uharibifu, na kuongeza kuwa serikali itachukua hatua za kisheria kwa
yeyote atakayebainika kuhusika na uhalifu huo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wanachama hao, waliwataka viongozi wa majimbo,
jumuiya na chama kwa ujumla kufanya ziara za mara kwa mara katika
mashina na Matawi ili kujua matatizo yanayowakabili wananchi pamoja na
ufanisi na udhaifu wa utekelezaji wa shughuli za kisiasa katika ngazi
hizo.
0 comments:
Post a Comment