NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kinaendekea na juhudi za kuishauri
serikali iharakishe utaratibu wa kutoa misaada kwa wananchi
walioathiriwa na maafa ya mvua ili waweze kupata huduma za msingi kama
walivyo wananchi wengine waliosalimika na tatizo hilo.
Kauli hiyo
imetolewa na Naibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar, Dkt.Abdalla Juma
Saadala '' Mabodi" katika mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maeneo
mbali mbali nchini yaliyopata maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha
nchini.
Dkt.Mabodi
aliwambia wananchi hao kwamba serikali ya Mapinduzi ya zanzibar
inayotokana na chama hicho ni sikivu na inathamini maisha na utu wa
wananchi wote bila ya kujali itikadi za kisiasa, hivyo itaendelea kutoa
mapendekezo kwa Idara ya Maafa nchini ifike kila pembe ya visiwa vya
zanzibar kuhakikisha wananchi wote waliopata maafa wanaratibiwa na
kupatiwa misaada.
Alieleza
kwamba pamoja na taasisi hiyo kufanya kazi za kisiasa bado ina jukumu la
kuwalinda na kuwasaidia wananchi wakati panapotokea majanga mbali mbali
ya kitaifa ili waweze kubaki salama na kuendelea na shughuli za
kimaendeo.
" Wananchi
tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atuvushe salama katika hii neema ya
mvua iliyochanganyika na mitihani, ili turudi katika maisha ya kawaida
na kuondokana na hofu.
Jukumu letu
kama chama cha kisiasa wakati wa maafa ni kuhakikisha kila mwananchi ana
kuwa salama na kupata huduma za msingi sambamba na kuwafariji huku
serikali ikiendelea kukamilisha taratibu za kutafuta ufumbuzi wa
kumaliza changamoto zinazotokana na maafa hayo." alieleza Dkt. Mabodi
wakati akitoa msaada wa fedha sh.200,000 kwa mwananchi wa Shehia ya
Miwani Unguja, Bw.Endward Maziku ambaye nyumba yake imebomoa na kukosa
makaazi ya kuishi.
Akitoa
ufafanuzi kwa wananchi wa maeneo ya shehia ya Miwani kuwa changamoto ya
miundo mbinu ya barabara inayowakabili , alisema SMZ ina mpango wa
kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa awamu pamoja na Vijiji vya Koani,
Jendele, Unguja Ukuu na Jumbi.
Alifafanua
kuwa baadhi ya barabara hizo tayari zilikuwa zimeanza kutengenezwa
lakini baadae serikali ikabaini kuwa Mkandarasi aliyepewa tenda hiyo
hana sifa na ikaamua kumfuta.
Sambamba na
hayo Naibu Katibu Mkuu huyo, aliendelea kuwasisitiza waakazi wa maeneo
mbali mbali kutibu maji kabla ya kuyatumia pamoja na kuwa karibu na
watoto wadogo wasicheze karibu na mabwawa ya maji ya mvua kwa lengo la
kuepuka athari za maafa.
" Nakiri
kwamba mvua hizi ni kubwa sana hazijawahi kutokea kwa miaka ya hivi
karibu, kwani mvua kama hizi nakumbuka zilitokea miaka ya 1972-1973 na
kuacha maafa makubwa.
Pia nawaomba
wanasiasa nchini tusitumie maafa haya kama ajenda ya kisiasa bali
tuwafariji na kutoa nasaha za kuwashauri mambo mema na kuwaeleza hali
halisi kwani SMZ na CCM hazipendi wananchi wapate majanga na
migogoro, hivyo mitihani hiyo ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu".alifafanua
Naibu Katibu Mkuu huyo.
Mapema
wananchi hao kwa nyakati tofauti walisifu kasi ya usimamizi wa Ilani ya
CCM inayotekelezwa na Serikali kwa kuimarisha huduma za msingi katika
sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi.
Akizungumza
Mkaazi wa Chwaka Wilaya ya Kati alisema licha ya kuwepo kwa changamoto
za maafa zilizoharibu miundombinu ya maji, barabara na umeme lakini bado
wana matumaini kwa serikali itafanya marekebisho ya haraka kwa baadhi
ya huduma ili zilidi katika hali ya kawaida.
Naye Mkaazi
wa Jambiani Kikadini, Ramadhan Kassim, aliwaomba wananchi wa maeneo
mbali mbali nchini kuwa na utamaduni wa kuwa na tahadhari ya kujipanga
mapema kwa kufuata ujenzi unaozingatia ushauri wa kitaalamu ili kuepuka
maafa wakati wa mvua zijazo.
0 comments:
Post a Comment