NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
ZAIDI ya Nyumba 300 katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi zimeathiriwa na Mvua za masika zinazoendelea kunyesha hivi sasa.
Akizungumza
katika mtaa wa ziwa maboga sheha wa shehia ya Tomondo, Bw. Mohamed Omar
Said alisema zaidi ya nyumba 200 katika eneo hilo zimeathiriwa na mvua
kwa kujaa maji na zingine kuporomoka.
Bw. Said alifafanua kwamba baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamehama katika makaazi yao na kuomba hifadhi katika maeneo mengine yaliyokuwa salama, huku idadi ya nyumba zinazoathiriwa na mvua hizo zikiendelea kuongezeka kadri mvua zinavyioendelea kunyenyesha.
Mbali na maeneo hayo pia katika mitaa ya Meli nne, Fuoni janga mizini na Fuoni Migombani kuna nyumba zaidi ya 100 zimeathiriwa na mvua hizo.
Akizungumza juu ya athari hizo, Mjumbe wa sheha wa shehia ya kibondeni, Bi. Zuhura Ame alisema hali za baadhi ya wananchi waliopata maafa hayo sio nzuri hivyo wanahitaji msaada wa dharura.
Alisema
kwamba licha ya viongozi wa majimbo hasa Wabunge, wawakilishi na madini
baadhi yao tayari wameanza kutoa msaada na wengine ndio wanajipanga
kufika kwa ajiri ya kuwafariji wananchi lakini bado panahitajika nguvu
za pamoja baina ya wananchi, vyama vya kisiasa na serikali ili kuinusuru
nchi kuingia katika maafa makubwa.
Naye
Mkaanzi wa Mwanakwerekwe, Mwajuma Salum aliomba serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kupitia Wizara inayohusika na masuala ya Miundombinu kutoa
kipaumbele cha kujenga madaraja makubwa na yenye viwango katika maeneo
mbali mbali nchini ili kuepusha hasara inayotokana na mvua hizo kila
mwaka.
“
Tumesikia juzi tu serikali yetu imetangaza bajeti ya mwaka inayofikia
Trioni moja, hivyo tunaomba kama inawezekana baadhi ya fedha zitumike
katika uimarishaji wa miundombinu yetu kwani wengi tunateseka kwa sasa,
mfano pale Mwanakwerekwe Gari za Shamba kuja mjini ni tabu kwani pale
katika Bwawa la maji hakupitiki.”, alisema Mwajuma.
Alisema
licha ya serikali kufanya ziara katika maeneo hayo bado baadhi ya
wananchi hawana makaazi ya kuishi hivyo wanaiomba serikali iwapatie
misaada ya dharura ili nao wapate huduma muhimu kwa kipindi hichi
kigumu.
Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” aliwaagiza viongozi wa Serikali za Mitaa Zanzibar kuacha tabia ya kuruhusu uuzaji wa viwanja na ujenzi katika
maeneo hatarishi hasa mabondeni na sehemu zinazotwaama maji ili kuepuka
athari za mafuriko zinazoweza kusababisha vifo na uharibifu wa mali.
Maelekezo hayo aliyatoa katika Mtaa wa Tomondo Ziwa maboga na maeneo mengine wakati katika ziara yake ya kuwafariji wananchi waliopata athari za mafuriko katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
Alisema wananchi
wanatakiwa kujenga utamaduni wa kujilinda dhidi ya maisha yao kwa
kuchukua tahadhari ya kutoishi katika maeneo wanayojua kuwa ni hatari
juu ya afya na maisha yao.
Aliahidi
kwamba CCM kwa kushirikiana na serikali inaendelea kutafuta ufumbuzi wa
kuwasaidia wananchi waliopata athari hizo kwa Unguja na Pemba.
“
Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi natoa pole sana kwa wananchi wetu wa
Zanzibar kwa Unguja na Pemba walioathiriwa na mvua hizi zinazoendelea
kunyesha hivi sasa, kwa upande wa CCM tutaendelea kuwa nanyi kwa kutoa
msaada wa Ari na Mali ili kuhakikisha mnarudi katika hali yenu ya
kawaida.
Pia
nakuombeni wananchi ifikie wakati na sisi tuisaidie serikali yetu kwa
kuepuka kuishi ama kununua sehemu ambazo tunajua kwamba hazifai kuishi
binadamu wakati mvua zinapoanza kunyesha.”, alisema Dkt. Mabodi na
kuongeza kwamba CCM itaendelea kuwa karibu zaidi na wananchi kwa lengo
la kuwapunguzia changamoto hizo.
Dkt.
Mabodi aliishauri serikali kuchukua hatua za haraka za kurekebisha
miundo mbinu ya barabara, maji na umeme kwa baadhi ya maeneo yaliyokubwa
na mafuriko hayo ili wananchi waendelee kupata huduma muhimu za
kijamii.
Aidha alitoa wito kwa wananchi ambao kwa sasa makaazi yao bado yapo salama kujitolea kwa kuwasaidia wenzao waliopata maafa huku Chama kwa kushirikiana na serikali wakitafuta njia mbadala za kusaidia katika maeneo hayo.
Sambamba
na hayo aliitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kutembelea katika
maeneo yaliyopata athari hizo kwa kugawa dawa za kutibu maji ya kunywa
sambamba na kutibu visima ambavyo maji yake hayo salama kwa lengo la
kuwanuru wananchi wasipate maradhi ya miripuka kwa kipindi hichi cha
kuelekea katika Mwezi wa Ramadhani.
Alisema sululisho la kumaliza tatizo la maafa hayo yanayotokea kila mwaka ni lazima wananchi waache kujenga katika mitaro ya kusafirisha maji, hali inayosababisha maji hayo kukosa njia za kupita na kuwaathiri wananchi wengine wasiokuwa na hatia.
Naibu Katibu Mkuu huyo, Dkt. Mabodi katika ziara hiyo amefuatana na uongozi wa Mkoa wa Magharibi na Wilaya ya Dimani akiongozwa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa Mkoa huo , Yussuf Mohamed Yussuf na alitembelea maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi mengi yakiwa katika Wilaya ya Maghatibi ‘’B” ambayo ni Tomondo, Mwanakwerekwe Sokoni, Mwanakwerekwe Meli nne, Fuoni Migombani na Fuoni Chunga.
0 comments:
Post a Comment