Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NA IS-HAKA OMAR-ZANZIBAR.
JUMLA
ya Pikipiki 14 aina ya Vespa zenye thamani ya shilingi milioni 37
zimetolewa na Mbuge wa jimbo la Kiwengwa Khamis Mtumwa kwa Makatibu wa
Matawi ya CCM ya jimbo hilo.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi hivyo huko katika uwanja wa
mpira wa kwa Gube, mbunge huyo alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020
kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.
Alieleza
kwamba lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuwarahisishia huduma za usafiri
watendaji hao ambao muda mwingi wanakuwa na majukumu mbali mbali
yanayohitaji usafiri wa haraka ili yaweze kutekelezwa
kwa wakati.
Aliahidi
kuwa hiyo ni sehemu tu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jimbo
hivyo ataendelea kutatua kero mbali mbali zinazowakabili wananchi wa
jimbo hilo.
“
Nitaendelea kumarisha huduma mbali mbali za kijamiii kadri mwenyezi
mungu atakavyonijaalia, wito wangu kwenu ni kwamba miradi ambayo kwa
sasa naitekeleza katika jimbo hili mnatakiwa kuitunza
ili iweze kuwanufaisha watu wote.”, alisisitiza Khamis.
Akizungumza
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla
‘Mabodi’ mara baada ya kukabidhi Pikipiki hizo kwa watendaji hao
aliwataka viongozi wa majimbo ya chama hicho
kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo kwa
wananchi.
Alisema
kwa sasa viongozi wanatakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa vitendo ili wananchi waone
maendeleo yanayofanywa na viongozi wao.
Alisisitiza
kuwa ni lazima viongozi wa majimbo waende na wakati Kwa kutangaza na
kutoa taarifa za uhakika juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM , hatua
itakayosaidia kujenga imani za wananchi waliowachagua
katika uchaguzi mkuu uliopita.
“
Naendelea kuwakumbusha baadhi ya wabunge, wawakilishi na madiwani ambao
bado utekelezaji wao wa Ilani ya Chama chetu unasuasua katika majimbo
yao kuwa waanze kurudi kwa wananchi kutekeleza yale
waliyowaahidi kabla ya uchaguzi mkuu ujao”, alisema Dkt. Mabodi.
Nao
baadhi ya makatibu mbali mbali waliokabidhiwa vifaa hivyo wameahidi
kuvitumia vizuri kwa lengo la kuimarisha shughuli mbali mbali za chama
hicho.
0 comments:
Post a Comment