Home » » Rais wa Zanzibar na mkewe washiriki katika zoezi la kupata vitambulisho vya Taifa

Rais wa Zanzibar na mkewe washiriki katika zoezi la kupata vitambulisho vya Taifa

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiwa katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi kushiriki katika zoezi ya upigaji wa picha za vitambulisho vya Taifa, sambamba  na utiaji saini fomu maalum na kuweka  alama za vidole,ikiwa ni utaratibu  wa ukamilishaji wa zoezi hilo. Aliyesimama kuwaelekeza ni Mkurugenzi wa Vitambulisho


vya Taifa Zanzibar Bw,Vuai Mussa Suleiman


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati)  akiweka  alama za vidole,baada ya kupiga picha za vitambulisho vya Taifa,sambamba utiaji saini fomu za ukamilishaji wa zoezi hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa Zanzibar Bw. Vuai Mussa Suleiman, na kulia ni Bw Mathayo Sungu wa NIDA.  
Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa