Home » » Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali wa Zanzibar awataka wakurugenzi na watendaji wampe ushirikiano.

Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali wa Zanzibar awataka wakurugenzi na watendaji wampe ushirikiano.


Na Hamad Hija Maelezo.
Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali wa Zanzibar Ali Juma Shamhunna amewataka Wakurugenzi na watendaji wa wizara hiyo kumpa ushirikiano wa hali ya juu ili aweze kutekeleza majukumu ya wizara yake hiyo mpya ipasavyo

Amesema kwa hivi sasa anahitaji msaada kutoka kwao ili kazi zake atakazo zifanya akiwa waziri wa elimu na mafunzo ya amali ziwe rahisi katika kutekeleza majukumu yake katika wizara hiyo

Shamhuna aliyasema hayo  hapo jana huko Wizara ya elimu  na mafunzo ya amali Mazizini wakati wa makabidhiano ya Wizara  hiyo na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Ramadhan Abdulla Shaaban ambaye alimkabidhi wizara hapo jana

Aidha alisema mbali na msaada ambao anauhitaji katika wizara hiyo kutoka kwao pia anahitaji mashirikiano makubwa ambayo yatamfanya afanye kazi zake kwa urahisi zaidi katika wizara yake hiyo mpya kwa sasa Alisema anategemea mashirikiano zaidi kutoka kwao pindi wasipompa mashirikiano watakuwa wanamueka mahali paya katika kuifanyia kazi wizara hiyo ambayo ndio kwanza anakabidhiwa

Aidha Shamhuna alisema kuwa amekubali kuchukuwa jukumu hilo gumu  na zitolakini alisema atafanya kazi yake hiyo kwa nguvu na moyo wake wote katika kipindi chake cha kazi hiyo ya kuwa waziri katika wizara hiyo

Aidha Ali Juma Shamhuna katika sehemu yake ya mazungumzo hayo ya kukabidhiwa wizara hiyo waziri huyo wa elimu alisema pia anahitaji uvumilivu wa hali ya juu kutoka kwa viongozi wa wizara hiyo alisema kuwa wakurugenzi wa wizara hiyo ni watu wataalam hivyo anategemea sana mafanikio makubwa kutoka kwao

Naye aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Ramadhan Abdulla Shabaan amemkabidhi wira hiyo ikiwa na idara saba na amemkabidhi wizara kwa moyo mkunjufu na yupo tayari kutowa ushirikiano naye katika utekelezaji wa majukumu ya kazi yake hiyo  

Waziri Shaaban   wa zamani wa wizara hiyo alisema kuwa atampa ushirikiano wowote na wakati wowote ili aweze kumrahisishia kazi yake hiyo ya hivi sasa

Kukabidhiwa kwa wizara kwa  waziri huyo mpya wa wizara ya elimu na mafunzo ya amali kutokana na mabadiliko aliyoyafanya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohd Shein ambapo kati ya mabadiliko hayo alimteua Ali Juma Shamhuna kuwa waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar

Wakati huo huo aliyekuwa waziri wa habari utamaduni utalii na michezo Abdilah Jihad Hassan leo amemkabidhi wizara na majukumu ya wizara hiyo waziri mpya wa wizara hiyo Said Ali Mbaruok ambapo baada ya kukabidhiwa wizara hiyo aliutaka uongozi wa weizara hiyo kumpa ushirikiano katika utendaji wake wa kazi

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa