Home » » ZIARA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR KATIKA KANISA LILILOCHOMWA MOTO

ZIARA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR KATIKA KANISA LILILOCHOMWA MOTO


Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson
D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Mohd Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto
katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30
wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.


PICHA NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud
akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God
Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa
Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni  Mkuu wa Jeshi
la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson
D,Kaganga akielezea  kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile
kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea
Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa
na tokeo hilo.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson
D,Kaganga akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa
ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mohd Aboud baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea
Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa
na tukio hilo.
-Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman
Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na
Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu
mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo
limechomwa moto.

Mku wa Jeshi la Polisi IGP Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na
baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of
God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na
baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa
Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi
Zanzibar Mussa Ali Mussa.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa
hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na
Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka
kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa