Home » » Chama cha CUF chawataka wananchi wa Zanzibar kutulia na kupisha Serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu

Chama cha CUF chawataka wananchi wa Zanzibar kutulia na kupisha Serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu



Na Juma Mohammed,
MAELEZO Zanzibar.

Chama cha Wananchi(CUF) kimewataka wananchi kutulia na Serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar.

Taraifa ya Chama hicho kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma,Salim Bimani ilisema “Chama cha CUF kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila jazba na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mawazo yao”

Taarifa hiyo ilisema kwamba vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa moto na kuharibu mali za watu ni bvya uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa Kizanzibari.

“Uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria bila uonevu wala upendeleo” Alisema Bimani katika taarifa yake hiyo ambayo pia alisema kwamba ni lazima kwa wakati huu na kwa haraka iwezekanavyo, Serikali izungumze na Mashekhe bila ya kuona muhali na kwa uwazi kabisa ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa faida ya nchi.

Chama hicho kimesema kwamba pamoja na sababu au visingizio mbalimbali vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwemo za hamasa za wananchi, chuki binafsi, ukosefu wa hekima,matumizi ya nguvu za dola na hata uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutokupendelea maridhiano ya kisiasa Zanzibar.

“Chama cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania,hakiwezi kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar wakibainika kufurahia mazingira hayo,kwa maslahi binafsi na pia kutoa kauli za kutatanisha za kisiasa” Alisema Bimani katika taarifa yake.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa