Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib
Fereji akitoa taarifa rasmi ya serikali kuhusiana na maadhimisho ya
mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanayofikia kilele chake tarehe
26/06/2012 kila mwaka.Picha na Hassan Hamad-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
Fereji akitoa taarifa rasmi ya serikali kuhusiana na maadhimisho ya
mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanayofikia kilele chake tarehe
26/06/2012 kila mwaka.Picha na Hassan Hamad-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
---
Janatarehe 26/06/2012, ni siku ya maadhimisho ya mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya duniani. Tamko la kimataifa kuhusiana na matumizi ya dawa za kulevya ni kwamba
bado dawa za kulevya zinaendelea kuathiri afya za binadamu na ndio maana
juhudi za mapambano hayo zikaendelezwa.
bado dawa za kulevya zinaendelea kuathiri afya za binadamu na ndio maana
juhudi za mapambano hayo zikaendelezwa.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari huko ofisini kwake
Migombani Mjini Zanzibar, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais Fatma Abdulhabib Fereji amesema vita dhidi ya dawa za kulevya ni
ngumu sana, lakini inawezekana iwapo jamii itashirikiana dhidi ya
mapambano hayo.
“Hii ni kutokana na ukweli kuwa wanaojishughulisha na biashara hii ni
watu wenye fedha nyingi na ujanja kupita kiasi, inafika wakati watu hawa
wanashusha mzigo baharini na kwenda kuuzamia kwa wakati wao na
kuupeleka wanakokujua wao. Na kama wakiamua kuhonga hawahongi laki moja
au mbili, hesabu hiyo inakuwa kwa dola, sasa fikiria”, aliweka wazi Mhe.
Fatma Fereji.
Hata hivyo amesema serikali inajitahidi kuongeza nguvu za kupambana na
uingizaji na matumizi ya dawa hizo, sambamba na kusaidia kupata hifadhi
na mafunzo ya amali kwa vijana walioamua kuachana na dawa hizo.
Amesema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na serikali hadi sasa ni
pamoja na kutenga shilingi milioni mia moja kwa ajili ya matayarisho ya
ujenzi wa nyumba za kuwaendeleza vijana walioamua kuachana ya dawa za
kulevya (sober houses) huko Tunguu ambazo zikimalizika zitatoa huduma
zote bure kwa vijana hao.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Tujenge jamii yenye afya
bila ya dawa za kulevya”.
0 comments:
Post a Comment