Home » » TTCL yatoa msaada katika skuli ya Chokocho mkoani Pemba

TTCL yatoa msaada katika skuli ya Chokocho mkoani Pemba

Mkuu wa Biashara kanda ya Zanzibar Bw. Husssein Nguvu akimkabidhi simu
za mkononi Mkuu wa polisi wa Wilaya Mkoani-Pemba Muhidin Juma Mohamed.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Polisi Jamii Jondeni Sheha M. Sheha
Baadhi ya Maafisa wa TTCL wakibadirishana mawazo.
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imetoa msaada wa vitu mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mifuko ya saruji, nondo pamoja na mchanga katika skuli ya Chokocho mkoani Pemba.

Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Biashara wa Kanda ya Zanzibar inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara Bw. Hussein Nguvu amesema, TTCL ina vipaumbele vingi lakini wameamua kuchangia katika shule kwani wanatambua Elimu ni Mlima, kadri unavyozidi kupanda, ndivyo unavyozidi kuona mbali.

Naye mwalimu mkuu wa skuli ya Chokocho Bw. Idrisa Daudi Ame amesema, wanashukuru sana kwa msaada huo kwani utaleta ahueni katika shule hiyo iliyo na changamoto nyingi ikiwamo uchakavu kwani ilianzishwa miaka mingi iliyopita.

Wakati huo huo, Mkuu huyo wa kanda ya Zanzibar Bw. Hussein Nguvu amekabidhi Vifaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na simu za mkononi, viatu vya tope (gum boots) makoti ya mvua (rain coats), vizibao (Reflective jackets) tochi pamoja na filimbi kwa Polisi Jamii Jondeni mjini Pemba.

Akiongea wakati wa kupokea vifaa hivyo Mkuu wa polisi wa Wilaya Mkoani Pemba Muhidin Juma Mohamed ameishukuru kampuni ya TTCL kwa kushirikiana na Jeshi la polisi na hasa Polisi jamii, kwani ulinzi unaenda sambamba na mawasiliano, hivyo simu hizo na vifaa vingine vitawasaidia sana kiutendaji.

Naye mwenyekiti wa Polisi jamii Jondeni Bw. Sheha M. Shaha amesema, anaishukuru TTCL kwa msaada huo kwani utawaongezea ufanisi katika utendaji wa kazi pia amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwa karibu na jamii na hasa kiutendaji, na ndio maana wamefanikiwa kufika hapo walipo na wanaweza kufanya kazi kiufanisi bila shuruti.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa