Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Edgar Senga akiwasilisha mada ya majukumu ya idara hiyo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa ya Zanzibar walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Operesheni na Huduma za Binadamu Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib akiwasilisha mada ya majukumu ya Kamisheni hiyo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akifafanua jambo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa ya Zanzibar walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam, wengine ni waratibu wa maafa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.
Kamisheni
ya Kukabiliana na maafa Zanzibar imevutiwa na shughuli za kuratibu
maafa nchini zinazofanywa na serikali ya awam ya Tano kupitia Ofisi ya
Waziri Mkuu,Idara ya Kuratibu maafa ikiwa ni pamoja na kuratibu Afya
moja ambapo katika Dhana ya Afya Moja, sekta ya afya ya binadamu,
wanyama (pori na wafugwao) na mazingira, zinakuwa na mawasiliano ya
karibu kiutendaji na kupanga mikakati ya pamoja katika kujiandaa na
milipuko ya magonjwa na kukabiliana nayo endapo itatokea.
Akiongea
wakati wa ziara ya Kubadilishana Uzoefu na Idara ya Kuratibu Maafa na
Ofisi ya Waziri Mkuu,jijini Dar es salaam leo tarehe 15 Novemba 2017,
Mkurugenzi Mtendaji Kamishseni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Shaban
Mohamedi amebainisha kuwa kamisheni yake imevutiwa na jinsi idara ya
maafa inavyoweza kuimarisha juhudi na ushirikiano wa sekta mbalimbali
katika maandalizi ya kuzuia,kujiandaa na kukabili magonjwa ambukizi kwa
kujumuisha sekta zote muhimu.
“Tutaupitia
mpango mkakati wa Afya moja ili nasisi tuanze juhudi za kuratibu Afya
moja kwani Kamisheni inajukumu lakukabiliana na Maafa hivyo tutachukua
juhudi za kuhakikisha na sisi Zanzibar tunashirikiana na wadau husika
ili tuweze kutumia rasilimali ndogotulizonazo kuweza kukabili magonjwa
yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu yanayoiathiri jamii ya
Zanzibar” alisisitiza Khatibu
0 comments:
Post a Comment