Imeandikwa na Maulid Ahmed, Dodoma
Amesema kauli kama hiyo ilitakiwa kutolewa na watu wa vijiweni na si kiongozi kama huyo. Profesa Mbarawa alisema hayo kuhusu Saada ambaye ni Mbunge wa Welezo kwa tiketi ya CCM, wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa mwaka 2017 uliopitishwa na wabunge na unasubiri kusainiwa na Rais John Magufuli uwe sheria.
Saada wakati anachangia muswada huo alitaka shirika hilo liwe na sura ya Muungano zaidi kwa kuwekwa Mkurugenzi Mkazi wa shirika kwa upande wa Zanzibar na awe Mzanzibari ili kusaidia kupata ushirikiano kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na balozi mbalimbali zilizopo visiwani humo.
“Nimeshtushwa na sikutegemea Saada aseme maneno hayo kwani amekuwa serikalini tena kiongozi mkubwa, maoni yake nilitegemea yasemwe na mtu wa kijijini kule Pemba au vijana wa kijiweni darajani (Unguja).
Kauli hiyo ni ya kibaguzi na nina imani SMZ itamuunga mkono mtendaji yeyote wa shirika hilo atakayekuwa madarakani kwani Mtanzania yeyote anaweza kufanya kazi kokote,” alisema. Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alisema kauli ya Saada ni kuanzisha ubaguzi.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment