Wakazi
wa kijiji cha Mzuri -Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika
mradi wa kitalu cha miti moja ya mradi ulioibuliwa na walengwa wenyewe
kupitia PWP unaoendeshwa na TASAF ambapo walengwa hulipwa fedha kwa kazi
hiyo.
Kitalu
cha miti kilichotayarishwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya
maskini kupitia mpango wa ajira za muda wa TASAF wenye lengo la
kuwaongezea kipato kwa kuwalipa kulingana na ushiriki wao katika kazi
hiyo.
Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa
na TASAF wakishiriki katika kazi za kutayarisha kitalu cha miche ya
miti katika kijiji cha Mzuri -Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja.
Mfuko
ya miche ya miti iliyotayarishwa na wakazi wa kijiji cha Mzuri
Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya kujaza
udongo ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa ajira za muda PWP unaotekelezwa
na TASAF.
Kazi
ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini -Makunduchi mkoa wa
kusini Unguja ambayo ni moja ya mkakati wa TASAF wa kuwaongezea kipato
walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia ajira ya muda PWP.
Baadhi
ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF
katika kijiji cha Kijini Makunduchi mkoa wa kusini Unguja wakishiriki
katika kazi za ujenzi wa barabara kupitia mpango wa ajira za muda PWP.
Walengwa
wa mpango wa kunusuru kaya maskini katika eneo la Kijini Makunduchi
mkoa wa kusini Unguja wakiwa katika harakati za ujenzi wa barabara
kupitia mpango wa ajira za muda PWP kupitia TASAF.
Barabara
inayojengwa kupitia mpango wa ajira ya muda PWP ambapo walengwa wa
Mpango wa Kunusuru kaya maskini kupitia TASAF wakiwa katika eneo la
mradi wa barabara yenye urefu wa kilometa Moja .
Walengwa
wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii TASAF wameanza utekelezaji wa miradi ya ajira za muda na kisha
kulipwa ujira katika miradi wanayoibua kwenye maeneo yao .
Walengwa
wa vijiji kadhaa vilivyoko kwenye Mpango huo kikiwemo kile cha Mzuri na
Kijini vilivyoko katika eneo la Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja
wameanza kutengeneza barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa moja na
vitalu vya miche ya miti ya asili na matunda katika eneo lao na kisha
kulipwa fedha chini ya utaratibu ulioandaliwa na TASAF ambao ni moja ya
mkakati wa kuwaongezea kipato walengwa na kupambana na umaskini.
Akizungumza
na timu ya waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo Sheha wa eneo
hilo Bwana Mwita Masemo Makungu amebainisha kuwa mpango huo umeitikiwa
vizuri na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika eneo hilo
na kuwa jitihada hizo za TASAF zimeamsha ari ya wananchi kujiletea
maendeleo kwenye maeneo yao na kupunguza kero ya barabara iliyokuwa
inawakabili.
Hata
hivyo Bwana Makungu amesema pamoja na ushiriki wa wananchi kwenye kazi
hiyo kupitia mpango wa ajira za muda bado wananchi hao wanakabiliwa na
tatizo la vifaa na utaalamu hususani katika ujenzi wa barabara ambao
unahitaji vifaa vizito ambavyo havipo kwenye maeneo yao na hivyo kuomba
serikali kuona namna ya kukamilisha kazi hiyo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment