Home » » WANAFUNZI 686 WA CHUO KIKUU CHA ELIMU CHA KUMBU KUMBU YA DR. ABDULRAHMAN AL – SUMAIT WATUNUKIWA VYETI VYAO LEO ZANZIBAR

WANAFUNZI 686 WA CHUO KIKUU CHA ELIMU CHA KUMBU KUMBU YA DR. ABDULRAHMAN AL – SUMAIT WATUNUKIWA VYETI VYAO LEO ZANZIBAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait wakiingia kwenye uwanja kwa ajili ya Mahfali ya 15 ya chuo hicho hapo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ambae alimuwakilisha Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kwenye Mahafali hayo ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Hicho Dr. Abdulrahman Al - Muhailan na kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Hamed Rashid Hikmany.


 Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait wakiingia kwa maandamano kwenye uwanja kwa ajili ya kupewa stashahada zao.
  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait, Dr. Abdulrahman Al – Muhailan akitoa salamu kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho hapo chukwani.
  
 Balozi Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Shein akimkabidhi zawadi mwanafunzi Bora wa Daraja la kwanza katika Fani ya Kiarabu na Dini Kijana Nuru Ally Nassor Muhanna.
 Balozi Seif Ali Iddi akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho Dr. Abdulrahman Al – Muhailan kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho hapo chukwani.
 Seif pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho Dr. Abdulrahman Al – Muhailan wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa mahfali ya 15 ya wahitimu 686 wa chuo hicho. Aliyepo kati kati yao ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuni.


 Balozi Seif akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kubmu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait, Dr. Abdulrahman Al – Muhailan hapo Chukwani.Wa kwanza kulia anayeshuhudia maagano hayo ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Hamed Rashid Hikmany.



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema Vyuo Vikuu Nchini licha ya kuendelea kutoa taaluma kwa vijana wa elimu ya juu lakini bado vina wajibu na jukumu kubwa la kuhakikisha wasomi wake wanatumia vipaji vyao katika kufanya tafiti kwenye maeneo mbali mbali.

Alisema tafiti hizo zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwa wasomi wachanga wanaoanza kupata taaluma kwenye Vyuo hivyo sambamba na kuliwezesha Taifa kupiga hatua za haraka za Maendeleo.

Dr. Ali Moh’d Shein alitoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya 15 ya Wahitimu 686 wa digrii ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al - Sumait kiliopo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Alisema kuimarika kwa eneo la utafiti kutatoa fursa kwa wananchi mbali ya kupata elimu katika kiwango cha juu lakini pia watapata mbinu na maarifa ya kukabiliana na changamoto zilizowakabili maisha yao ya kila siku.

Rais wa Zanzibar alisema mchango mkubwa unaotolewa na Vyuo vikuu hapa Nchini hasa vile vyuo vikuu Binafsi umesaidia ongezeko kubwa la Walimu wa skuli mbali mbali za Sekondari hapa Visiwani.

Mapema Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al Sumait Chukwani Profesa Hamed Rashid Hikmany alisema kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa chuo hicho mwaka huu kimeongezeka mara dufu kutokana na mikakati mizuri iliyowekwa na Uongozi wa Chuo hicho.

Profesa Hikmany alisema malengo ya uongozi wa chuo hicho kwa sasa ni kuimarisha zaidi utoaji wa wanafunzi wenye kiwango bora zaidi utakaokidhi mahitaji ya taaluma kimataifa.

Akitoa salamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al - Sumait, Dr. Abdulrahman Al - Muhailan alisema Uongozi wa Chuo hicho utaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Sekta ya Elimu.

Dr. Al - Muhailan alisema hatua hii inalenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Wananchi wa Zanzibar na Kuweit kupitia sekta za mendeleo na ustawi wa jamii ambazo tayari zimeshaleta mafanikio makubwa kwa pande hizo mbili rafiki.

Jumla ya wanafunzi 686 wa fani za Sayansi, Sanaa, Lugha ya Kiswahili, Kiarabu mfunzo ya Dini ya Kislamu wamehitimu mafunzo yao na kukabidhiwa stashahada ya kwanza.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
19/1/2016.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa