Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT- Wazalendo, Khamis Iddi Lila
Pamoja na chama chake kumpiga ‘stop’, mgombea urais
wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT- Wazalendo, Khamis Iddi Lila, amesema
amekuwa akiomba dua usiku na mchana aibuke mshindi katika uchaguzi mkuu
wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu visiwani humo na
kwamba ina imani atashinda urais.
Lila amesema ana matumaini makubwa ya chama chake kufikia malengo
makubwa ya kisiasa visiwani humo baada ya kuibuka mvutano baina ya vyama
vikuu vya CCM na CUF juu ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka
huu na matokeo yake kufutwa na kusababisha CUF kususia uchaguzi huo wa
marudio.
Akizungumza mjini hapa mwishoni mwa wiki, Lila alisema mvutano wa
CUF na CCM una tija kubwa kwa vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo
kama wananchi watakubali kufanya mageuzi ya kukomesha ukiritimba wa
kisiasa katika visiwa vya Zanzibar baina ya vyama hivyo viwili.
Alisema pamoja na viongozi wa chama chake kutangaza kumsimamisha
uanachama kutokana na kushiriki uchaguzi huo wa marudio, bado
anajitambua kuwa mgombea halali baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kueleza kuwa wagombea wote
walioshiriki uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana ni wagombea halali katika
uchaguzi wa marudio.
“Mvutano wa CUF na CCM una neema na tija kubwa kwa vyama
vilivyobakia, ndiyo maaana naomba dua usiku na mchana nishinde urais wa
Zanzibar,” aliongeza kusema Lila.
UONGOZI WAMKANA
Hata hivyo, uongozi wa chama ACT -Wazalendo Zanzibar haumtambui
Lila kama mgombea wake na kama anashiriki uchaguzi huo atasimama kama
mgombea binafsi.
Msimamo huo ulitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Juma
Said Sanani, mjini Zanzibar jana, baada ya mgombea huyo kugoma kujitoa
katika uchaguzi huo wa marudio.
Alidai Lila amefukuzwa uanachama wa ACT-Wazalendo kutoka na na
kwenda kinyume na msimamo wa chama hicho wa kususia uchaguzi huo wa
marudio.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment