Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali
Iddi, amesema nguvu za pamoja ndio msingi wa kukabili matatizo ya
kuporomoka kwa kiwango cha elimu, ukosefu wa ajira kwa vijana na
unyanyasaji mkoa wa Kaskazini Unguja.
Ushauri huo aliutoa jana alipokuwa akiizindua Jumuiya ya Maendeleo
ya Mkoa wa Kaskazini Unguja (JMMK) katika hafla iliyofanyika Malindi,
Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema takwimu zinaonyesha wazi kwamba mkoa wa Kaskazini Unguja
unaongoza kwa kushuka kwa kiwango cha elimu na kuongezeka kwa vitendo
vya udhalilishaji, uchafuzi wa mazingira na mpasuko wa umoja
unaosababishwa na tofauti za kidini na kisiasa ambazo zimesababisha
kudidimia kwa hadhi na heshima ya mkoa huo.
“ Mkoa wetu hivi sasa umevamiwa na watu ambao wanatumia dini na
siasa kwa lengo la kuwagawa wananchi, mambo ambayo kama hawakuwa makini
watu hao wanaweza kuwaweka mahali pabaya wananchi wake,” alionya.
Alisema kipindi kirefu sasa shule za mkoa wa Kaskazini Unguja
hazifanyi vizuri katika mitihani ya kitaifa, hivyo kurudisha nyuma
maendeleo ya mkoa.
Balozi Seif aliitaka JMMK kujipanga vizuri kimpango na kimkakati
kwa upande ili kukuza kiwango cha elimu na hatimaye mkoa kurejesha hadhi
yake.
Alisema ili malengo hayo yafanikiwe vyema, jumuiya hiyo inahitaji
kuwa na ushirikiano wa karibu na viongozi wa shule zote zilizoko ndani
ya mkoa, wazazi, taasisi za kijamii na wanafunzi wenyewe.
kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za mikoa na Vikosi vya SMZ, Haji Omar Kheir, alisema nui
muhimu kwa wana jumuiya kujitolea nguvu zao ili kufikia malengo kwa
wakati muafaka.
Akizitaja changamoto zinazoendelea kujitokeza katika mkoa huo
kupotea kwa mila , silka na utamaduni ndani ya jamii na kuwa chimbuko la
kubuniwa kwa jumuiya hiyo ya Maendeleo ya Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini
Unaguja.
Wajumbe wa Bodi ya wadhamini wa Jumuiya hiyo Rais Mstaafu Dk Salmin
Amour Juma, Balozi Seif Ali Iddi, Fatma Bakari Mohamed, Ali Ameir
Mohammed na Rais Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye ni mjumbe wa heshima.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment