Home » » MKUTANO WA 10 WA KUTATHMINI SEKTA YA AFYA UNAOFANYIKA KILA MWAKA WAFUNGULIWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI

MKUTANO WA 10 WA KUTATHMINI SEKTA YA AFYA UNAOFANYIKA KILA MWAKA WAFUNGULIWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Muhammed Jidawi akiwakaribisha washiriki wa Mkutano wa siku tatu wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Mazizini.
Kiongozi wa washirika wa maendeleo kutoaka Mashiriki ya Umoja wa Mataifa DKT. Kirsten Havemann akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar unaofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Baadhi ya washirika wa maendeleo na maafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua Mkutano wa 10 wa kutathmini maendeleo ya sekta ya Afya Zanzibar kwa niaba ya Rais wa Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiteta jambo na kiongozi wa washirika wa maendeleo kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Dkt. Kirsten Havemann wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar.
Mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi na washiriki wa maendeleo na maafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar mara baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku tatu wa kutathmini sekta ya Afya unaofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa