Home » » GRAND MALT KUMWAGA VIFAA LIGI KUU ZENJI LEO

GRAND MALT KUMWAGA VIFAA LIGI KUU ZENJI LEO


na Mwandishi wetu
WADHAMINI wa Ligi Kuu ya soka Zanzibar, kinywaji cha Grand Malt, leo wanatarajiwa kukabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam, alisema, hafla ya kukabidhi vifaa hivyo itafanyika katika hoteli ya Zanzibar Ocean View, kuanzia saa 4 asubuhi na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk.
Meneja huyo alisema timu zote 14 zinazoshiriki ligi hiyo, zitakabidhiwa vifaa, ikiwemo jezi na mipira kwa ajili ya kufanikisha ushiriki wao.
“Kila kitu kinakwenda sawa na tumepanga kukabidhi vifaa kesho (leo), kwani tunataka tuwe na ligi yenye ushindani mkubwa.
Grand Malt, imejitolea kwa kila hali kuhakikisha inakuza michezo Zanzibar na hasa ukichukulia, ni muda mrefu ligi yao ilikuwa haina udhamini wa uhakika,” alisema.
Grand Malt, kinywaji kisicho na kilevi, ndio ambao wameingia udhamini wa ligi hiyo inayosimamiwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA).
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa