Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea
kuridhishwa kwake na uwepo wa vyakula na matunda yenye viwango kwa ajili
ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Hata hivyo alisema bei zake bado ziko juu ikilinganishwa na kipato cha wananchi, na kwamba wananchi walio wengi wanashindwa kumudu kununua bidhaa hizo.
Maalim Seif alitoa kauli hiyo katika ziara yake ya kutembelea masoko mbali mbali ya manispaa ya mji wa Zanzibar, kuangalia hali ya upatikanaji wa bidhaa na matunda, ambayo hutumika katika mwezi wa Ramadhan.
Aliwashauri wakulima na wafanyabiashara kuzingatia hali za maisha ya wananchi, na kuangalia uwezekano wa kupunguza bei, ili wananchi waweze kumudu kununua bidhaa hizo.
Alisema serikali imetoa fursa ya soko huria kwa wafanyabiashara, na kwamba upandaji wa bei kwa bidhaa hizo unatokana na wakulima na wafanyabiashara wenyewe.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa vitoweo, Maalim Seif alisema hali hairidhishi, kwa vile samaki waliopo ni wachache, na hivyo kuuzwa kwa bei ya juu.
Aidha Maalim Seif alielezea kuridhishwa na maendeleo ya soko la Mombasa ambalo linaendelea kufanyiwa matengenezo makubwa ambayo yatasaidia kutunza hadhi ya soko hilo la matunda.
Hata hivyo, alielezea kutoridhishwa na hali ya usafi katika soko la samaki Malindi, na kuliagiza Baraza la Manispaa kuweka utaratibu mzuri wa kulitunza eneo hilo la kuuzia samaki, ili liwe katika hali ya usafi wakati wote.
Baadhi ya wafanyabiashara wameiomba serikali kuwawekea mazingira bora ya kufanya biashara zao, sambamba na kulalamikia baadhi ya wafanyabiashara waliorejea soko la Mwanakwerekwe baada ya kuhamishiwa katika soko la Mombasa.
Katika ziara hiyo Maalim Seif alitembelea soko la matunda Mombasa, soko Kuu la Mwanakwerekwe, Kituo cha biashara Saateni na Soko Kuu la Darajani.
Wakati huo huo Maalim Seif aliwatembelea na kuwafariji watoto yatima wanaolelewa na jumuiya ya Muzdalifat katika eneo la Amani mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdallah Hadhir Abdallah aliishukuru serikali kwa mashirikiano waliyonayo kwa jumuiya hiyo, na kuiomba kuongeza misaada yake ili kuwaendeleza watoto yatima wanaolelewa katika vituo mbali mbali vya Zanzibar.

SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment