Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuagiza Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar { ZIA } kuwa wabunifu katika kutoa huduma zinazokwenda kimataifa baada ya kufanya ziara ya ghafla katika uwanja huo.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwnja wa Ndege wa Zanzibar Nd. Said Iddi Ndombogani na Katibu Mkuu Wizara ya Maiundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akili.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Nd. Said Iddi ndombogani kulia akimpatia maelezo Balozi Seif aliyepo kati kati wakati alipofanya nziara ya ghafla kiwanjani hapo.
Kulia yao ni Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akili.
Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akili akimfafanulia jambo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipofanya ziara fupi kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Baadhi ya abiria wa Kimataifa walioingia Zanzibar kwa usafiri wa anga wakipata huduma zitakazowapa fursa za kuwepo nchini kwa taratibu zilizowekwa kisheria.
Balozi Seif akiagizwa kuandaliwa utaratibu wa utoaji huduma wa ubia kwa watendahji wa uwanja wa ndege wa Zanzibar ili kupunguza msongamano wa abiria kiwanjani hapo.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
******
******
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi
pamoja na Watendaji wa Mamlaka ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Zanzibar { ZIA } kuwa wabunifu katika kuandaa utaratibu mzuri unaokwenda
na wakati ambao utaondoa usumbufu kwa wasafiri wanaotumia uwanja huo.
Alisema
watendaji hao pia wanapaswa kubadilika na kwenda na wakati kulingana na
huduma wanazotoa kwa wasafiri hasa wakizingatia kwamba uwanja huo
hivi sasa unaendelea kuimarishwa katika hadhi na kiwango cha
Kinachokubalika kimataifa.
Balozi
Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati alipofanya ziara fupi ya ghafla
kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kufuatia malalamiko
mbali mbali aliyokuwa akiyasikia kutoka kwa baadhi ya abiria kutokana na
huduma zinazotolewa uwanjani hapo .
Balozi
Seif alisema utaratibu uliopo hivi sasa ni vyema ukaimarishwa zaidi
ili kupunguza bughdha pamoja na kuwapa faraja abiria ambao wengi kati
yao huwa tayari wameshachoka kutokana na uchovu wa safari zao za
Kimataifa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar uliutaka uongozi huo wa Mamlaka ya Uwanja
wa Ndege wa Zanzibar kukaa pamoja na Idara ya Uhamiaji pamoja na taasisi
nyengine zinazokusanya mapato kiwanjani hapo katika kulitafutia
ufumbuzi wa haraka tatizo la urasimu unaosababisha msongamano mkubwa wa
wasafiri.
Mapema
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Zanzibar Nd. Said Iddi
Ndombogani alisema mamlaka hiyo inaendelea na juhudi za kukamilisha
matengenezo ya banda la wasafiri ili kuondosha malalamiko ya abiria
kuteremka mbali na eneo la kupata huduma zingine.
Alifahamisha
kwamba Mamlaka inaendelea kuzingatia vigezo vya Kimataifa katika kutoa
huduma kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa anga ambao humtaka abiria
anayesafiri ateremke kwenye gari masafa ya mita mia Moja na eneo
analotakiwa kupata huduma kwa ajili ya safari yake.
0 comments:
Post a Comment