Unaweza
ukadhani ni ndoto lakini hii ni habari ya kweli baada ya Hifadhi ya
jamii NSSF kutangaza uwezekano wa kujengwa daraja la kihistoria zaidi
litakalounganisha Dar es salaam na Zanzibar.
Uwepo
wa daraja hilo unaweza kuwa ni neema kwa Watanzania wote na hata nchi za
jirani kwani itarahisisha shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa
asilimia kubwa kwa kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi.
Gazeti la HabariLEO liliripoti
kuwa kwa sasa Shirika hilo lipo katika mazungumzo na wataalamu
mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari
ya Dar kwa upande wa Bara na Unguja kwa upande wa Visiwani.
Mkurugenzi
mkuu wa NSSF Ramadhan Dau alisema ujenzi wa daraja hilo si ndoto bali
ni ukweli na tayari wameanza mazungumzo ya awali ili kutimiza malengo
yao.
Umbali
kati ya Dar na Zanzibar ni kilimeta73.43 sawa na maili45.62 hivyo
kuwepo na mradi huo ni jambo linalowezekana kwani kuna madaraja marefu
zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.
Kwa
sasa daraja refu zaidi duniani kote ni lile la Danyang-Kushan lililopo
nchini China ambalo lina umbali wa kilometa 165 sawa na maili102.4
ambalo lilifunguliwa Juni mwaka2011.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment