Dokta Gao Yun Lai akimpima presha na sukari bwana Mohd Ali, mkaazi wa Kisauni. PICHA NA ABDALLA OMAR – MAELEZO ZANZIBAR.
Dokta Fadhil Mohd ambae ni D0kta Dhamana Kanda ya Unguja akitoa maelezo kwa waadishi wa habari (hawapo pichani).
Wananchi mbalimbali wakipatiwa huduma za matibabu katika kijiji cha Kisauni Zanzibar.
Mwashungi Tahir Maelezo-Zanzibar
Jumla
ya madaktari bingwa tisa kutoka nchini china wakishirikiyana na
madaktari wa hapa Zanzibar wameweza kutoa huduma za afyakwa wananchi wa
shehia ya Kisauni kwa kuwapima na kuweza kujua afya zao na kuwapatia
huduma za matibabu.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi huko katika shehia ya Kisauni wilaya ya
Magharibi B Dr Fadhil Mohammed ambae ni dhamana ya kanda ya Unguja
amesema madaktari hao wamekuja kutoa huduma za afya za jamii hapa
Zanzibar.
Amesema
madaktari hao wanatoa huduma hizo vijijini kwa kila baada ya miezi
mitatu wanakwenda katika kijiji chengine kwa lengo la kuwarahisishia
huduma hiyo watu hao na kuwapelekea huduma hiyo katika maeneo yao.
“Lengo
ni kuwapelekea wananchi huduma hiyo karibu na maeneo yao ili waweze
kupata urahisi wa kuweza kujua afya zao” alisema daktari huyo.
Sambamba
na hayo Fadhil amesema jitihada hizi ambazo zinafanywa na madaktari hao
na kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ni kuweza kuimarisha huduma hiyo
kupitia vijijini ili kuweza kuwapa muamko wananchi na kuweza kujitokeza
kupima afya zao kwa urahisi.
Madaktari
hao bingwa ambao ni maspeshalisti wa maradhi mbalimbali wameweza
kuwapima wananchi maradhi mbali mbali na kuweza kuwapatia matibabu hapo
hapo bila ya usumbufu wowote.
Maradhi
wanayopima na kutoa huduma ni pamoja na ukimwi, koo, pua, meno, presha
magonjwa ya moyo , ganzi, sukari na matatizo ya mkojo na maradhi
mengineyo.
Pia
wanatoa huduma za akinamama za uzazi wa mpango kwa njia salama na
huduma za watoto ambapo akinamama wengi wameweza kujitokeza kwa
kujipatia huduma hiyo.
Nae
mratibu wa afya wa mama na mtoto Bi Fatma Ussi Yahya amesema
amefurahishwa sana na akinamama wa kijiji hicho pamoja na majirani kwa
kuweza kufika kwa wingi katika kujipatia na huduma hiyo.
Pia
kati ya madaktari hao bingwa Dr GAO YUNLAI amesema amefarijika sana
kuona wananchi wameweza kujitokeza kwa wingi na kupima vipimo vya aina
ya maradhi mbali mbali ikiwemo maradhi yasiyoambukuza ya kisuari na
presha.
Sheha
wa shehia hiyo ya Kisauni Hija Suleiman Othman amewataka wananchi wake
wasiidharau huduma hizi zinapofika vijijini kwani hiyo ni bahati adhimu
kwa wananchi wa visiwa hivi.
“Nimefurahi
kuona wananchi wangu wameweza kuhamasika kwa kujitokeza kwa wingi
kwenye huduma hizi ambazo wameletewa hapa hapa na pia huduma hizi
zinatolewa bure kupitia Wizara ya Afya.” Alisema sheha huyo.
Kwa
upande wa wananchi Bi M wanajuma Omar kutoka mitondooni amesema ameweza
kushiriki vizuri katika kujipatia vipimo na kuweza kujifahamu afya yake
ambayo vipimo vyote alivyoima ameweza kujigundua kuwa yuko salama .
Amewataka
akinamama na akinababa kuweza kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na
kuweza kujitambua na kupatiwa matibabu ambapo matibabu hayo yanatolewa
kwa wingi hapo hapo na kuweza kuwaambia kuwa kinga bora kuliko tiba.
Madakatari
hao ni maalum Chinese medical team wapo hapa visiwani kwa ajili ya
kutoa huduma kwa wananchi na kuweza kuwapa matibabu watu wote .
0 comments:
Post a Comment