Mwenyekiti wa Jumuiya ya
kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji)
akitoa maelezo ya Jumuiya na kumkaribisha mgeni rasmi (kushoto) Katibu
Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar Shekh. Abdalla
Talib kufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi
Sha-Ntimba Mombasa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanziba
Baadhi ya wanachama wa Jumuiya na
wageni walikwa wakisikiliza nasaha za Mwenyekiti wa Jumuiya ya
kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji)
hayupo pichani wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya Jumuiya
hiyo Dkt. Muh’d Hafidh akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza
kwa Mkutano. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
………………………………………….
Na Maelezo Zanzibar.
Taasisi za kiislamu nchini
zimeshauriwa kushawishi kuwepo kwa mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa Zaka
na Sadaka ili ziweze kuleta tija katika kundi kubwa la jamii ya Kislam.
Katibu mtendaji wa kamisheni ya
mufti namali ya amana Zanzibar sheikh abdalla talib amesema Lengo la
mfumo huo uliwekwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu ni kusadia na
kupunguza umasikini katika jamii lakini kwa sasa wengi wanaotaoa sadka
hizo hazifikii lengo hilo kwa vile kumekosekana mfumo bora unaowafikia
watu wengi na kuleta mabadiliko makubwa.
Akifungua mkutano wa jumuiya ya
zaka na sadaka Zanzibar ZASA ametolea mfano wan chi ya denmar amabyo ina
waislamu kwa asilimi 3 tu imekuw ana utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa
sadka na zaka hali iliyofanikisha kupatikana misaada mingi
iliyosaidia katika nchi hiyo na hata nchi nyengine.
Amefahamisha kuwa kwa kuwa
Zanzibar asilimia kubwa ya wanananchi wake ni waislamu ina nafasi ya
kufikia malengo hayo kama pia itatoa elimu kwa wananchi hasa wenye uwezo
ili kufahamu umuhimu wa Ibada hiyo pamoja na njia bora za kutoa zaka
na sadaka katika jamii.
Nae mwenyekii wa jumuiy hiyo
sheikh said masoud amesema kwa sasa umekuwa na mwamko mdogo hasa kwa
wafanyabiashara kutoa zaka na sadaka kulingana na taratibu zinazotakiwa
kidini.
Nae katibu wa jumuiya hiyo ya
jusaza omar abubakar Mohamed amesema jumuiya hiyo imeshatoa zaka kwa
watu 46 zikiwemo za fedha taslim, charahani, friza na wengine kujengewa
nyumba.
0 comments:
Post a Comment