Home » » Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Ashiriki Dua ya Kuuombea Mwili wa Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Asha Bakari Makame.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Ashiriki Dua ya Kuuombea Mwili wa Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Asha Bakari Makame.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia, Mama Salma Kikwete katikati, Mama Mwanamwema  Shein kushoto na Wananchi wa Zanzibar, wakiwa katika Dua ya Pamoja ya kumuombea aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia, Mama Salma Kikwete katikati, Mama Mwanamwema  Shein kushoto na Wananchi wa Zanzibar, wakiwa katika Dua ya Pamoja mbele ya Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. 
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wakishiriki kubeba Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame kabla ya mazishi yake yaliyofanyika  leo Januari 22,2016 katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto akizungumza na kuwafariji wanafamilia wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame baada ya Dua maalum iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe, Mhe. Asha amezikwa leo kijijini kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia akimfariji Mama Mzazi wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame, Bibi Mwanajuma Faki (90) wakati wa Dua maalum iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe Zanzibar, Mhe. Asha amezikwa leo kijijini kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto akizungumza na kuwafariji wanafamilia wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame baada ya Dua maalum iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe, Mhe. Asha amezikwa leo kijijini kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. Wa pili kushoto ni Mama Salma Kikwete katikati Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuagana na Wananchi waliofika kwenye Msiba wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa marehemu Asha Bakari Makame wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo Januari 22,2016 katika kijiji cha kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. (Picha na OMR)

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa