Serikali ya Marekani imeeleza masikitiko yake kufuatia uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza tarehe 20 mwezi machi kuwa siku ya uchaguzi wa marudio.
Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa kigezo kuwa tume ilichukua hatua bila kuwahusisha wadau wote kwenye mazungumzo ya kutatua mzozo wa kisiasa ulioikumba Zanzibar.
“Tunatoa wito kwa serikali ya Tanzania na Rais Magufuli kuhakikisha kumefanyika mazungumzo yanayohusisha pande zote ili kupata suluhisho la mzozo huo wa Zanzibar,” imesema taarifa hiyo iliyotiwa saini na msemaji wa wizara hiyo, John Kirby.
Aidha Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar imekwisha tangaza tarehe 20 March 2016 kuwa ni siku ya marudio ya uchaguzi tarehe ambayo imeungwa mkono na serikali ya Rais John Magufuli.
0 comments:
Post a Comment