Home » » Uchaguzi Zanzibar tarehe hadharani -ZEC

Uchaguzi Zanzibar tarehe hadharani -ZEC

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha ametangaza  tarehe ya  20 mwezi wa tatu 2016 kuwa ndiyo siku ya kurudia uchaguzi mkuu wa  Zanzibar.

Tangazo hilo lililotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibatr imebainisha kuwa wagombea wote walioteuliwa hapo awali ndio watakao kuwa wagombea katika uchaguzi huo.


Vile vile Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni.

Aidha Chama cha Wananchi (CUF) kimekuwa kikipinga kurudiwa kwa uchaguzi. Chama hicho mapema mwezi huu kilionya kwamba hatua hiyo inaweza kusababisha vurugu, huku chama cha Mapinduzi kikiwataka wanachama wake kujipanga kwa uchaguzi.

 

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa