Home » » Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na idara maalum za SMZ afungua mradi wa maji Makunduchi

Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na idara maalum za SMZ afungua mradi wa maji Makunduchi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

07
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Muh. Haji Omar Kheri akizungumza na wananchi wa Makunduchi katika ufunguzi wa mradi wa Maji safi, ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amewataka wananchi wa kijijihicho kushirikana na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) ili kuendeleza miundo mbinu hiyo na pia amewataka kuchangia kiasi cha pesa kwa wale watakao pata Maji.
01
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Muh. Haji Omar Kheri akisalimiana na wafanyakazi wa Mamla ya Maji Zanzibar (ZAWA) mara baada ya kufika Kijiji cha Makunduchi kufungua mradi wa Miji ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
02
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Muh. Haji Omar Kheri akifungua pazia pamoja na kufungua Maji kuashiria ufunguzi rasmin wa Mradi wa Maji safi katika Kijiji cha Makunduchi Mkoa kusini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
03
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Muh. Haji Omar Kheri akifungua pamoja na kufungua Maji kuashiria ufunguzi rasmin wa Mradi wa Maji safi katika Kijiji cha Makunduchi Mkoa kusini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
04
Tenki jipya la kuhifadhia Maji lililopo Makunduchi.
05
Baadhi ya wageni walikwa waliohudhuria katika ufunguzi wa Mradi wa Maji safi uliozinduliwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
06
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ali halili Mirza akitoa taarifa ya kitalamu wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Maji safi uliozinduliwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Tone multimedia company Limited
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa