Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman
akikunjuwa kitambaa ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya
Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.Ikiwa ni
shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman
akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili Zingwezingwe
Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya
Zingwezingwe.Ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 52 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman
akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya Zingwezingwe Mkoa wa
Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja,Ikiwa ni shamra shamra za
maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.kushoto ni Mke wa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi na kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Juma Kassim Tendwa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman
akipanda mti wa Mnazi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira katika Uzinduzi
wa Skuli ya Msingi ya Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya
Kaskazini B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi
ya Walimu pamoja na wanafunzi waliohudhuria katika Uzinduzi wa Skuli ya
Msingi ya Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B
Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Wanafunzi
Khadija Khamis kushoto na Asha Mahamudi kutoka Skuli ya Fujoni wakisoma
Utenzi katika Uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya Zingwezingwe Mkoa wa
Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za
maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.PICHA NA YUSSUF
SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
Na Ali Issa Maelezo –Zanzibar
Waziri
wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haruon Ali Suleiman
ameshauri walimu watakaosomesha Skuli ya Zingwezingwe wawe walimu
wanaoishi karibu na kijiji hicho.
Hayo
ameyasema leo huko Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini, Wilaya ya Kaskazini
‘B’ Unguja, wakati alipokuwa akifungua skuli mpya ya msingi ya kijiji
hicho ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar .
Ametaka
ushauri huo ufanyiwe kazi na iwapo watahitajika walimu wapya
kuajiriwa kwa ajili ya kufundisha katika skuli hiyo Wizara yake
ambayo ndiyo inayohusika na masuala ya ajira watakuwa tayari
kufanya hivyo.
“Ni
vyema kuajiri walimu wakaazi na wenyeji wa kijiji cha Zingwezingwe
wenye kuyaelewa mazingira ya kijiji hicho na mimi kama Waziri wa Ajira
niko tayari kusaidia hilo,” alisema Waziri Haroun.Aidha
aliwashauri wanafunzi wanaosoma katika skuli hiyo kuitumia frusa
waliyoipata kusoma kwa juhudi kwani hiyo ni skuli ya kwanza kujengwa
katika kijiji hicho.
Hata
hivyo aliwataka wazazi na walezi kwa upande wao kutimiza wajibu wao
wa kufuatilia kikamilifu maendeleo ya Watoto wao na kutoa ushirikiano
kwa walimu ili kufanikisha maendeleo ya watoto wao.Waziri
Haroun aliwataka walimu kusomesha kwa juhudi kwani serikali tayari
imeshatoa maelekezo ya kuwaongezea maslahi yao mara itakaporudi
madarakani baada ya uchaguzi wa marejeo.
Katika
kuongeza ujenzi wa madarasa mengine ya kusomea katika Skuli hiyo,
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utawala wa Umma alichangia
matofali 1000 ambapo ujenzi wake utaaza hivi karibuni.Nae
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi akitoa
salamu za Baloz Seif Ali Idd alisema suala la umeme katika skuli hiyo
litafanywa na Makamu huyo wa Rais.
Ujenzi
wa skuli hiyo yenye madarasa manne na Ofisi ya Mwalimu Mkuu
umegharimu shilingi milioni 66 ambazo zimetolewa na Shirika la
Maendeleo la Sweden SIDA, Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B, Mbunge
na Mwakilishi na Wazee wa kijii cha Zingwezingwe.
0 comments:
Post a Comment