Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amesema amekaa kimya kwa muda mrefu kuhusiana na suala la Zanzibar kwa
sababu Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar ni huru na hawezi kuiingia kwa namna
yoyote.
Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Diamond Jublee
jijini Dar es salaa alipokuwa akizungumza na watanzania wote kupitia
mkutano ulioandaliwa na wazee wa Jiji la Dar es salaam.
''Zanzibar ina tume yao ya uchaguzi ZEC kama ilivyokuwa Tanzania bara
tulivyo na NEC hivyo kama kuna ambaye hajaridhika na hali hiyo aende
mahakamani mahakama ndiyo itakayotoa tafasiri''amesema Dkt.Magufuli
Rais ameongeza kuwa ataendelea kukaa kimya kuhusu Zanzibar ili
wajiendeshe wenyewe kumaliza uchaguzi wao kama Tanzania bara
tulivyomaliza uchaguzi wetu salama
Aidha Rais amesema yeye kama amiri jeshi mkuu hatakubali chokochoko
yoyote Zanzibar au katika eneo lolote la nchi na yeyote atakae jaribu
kuleta vurugu vyombo vya usalama vipo makini na vitahakikisha amani na
usalama wa nchi unadumu siku hadi siku.
0 comments:
Post a Comment