Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Maalim Seif anasisitiza kwamba uchaguzi ulishafanyika na kukamilika
tarehe 25 Oktoba, 2015 na umethibitishwa na waangalizi wote kuwa ulikuwa
uchaguzi huru na wa haki. Waangalizi hao ni pamoja na wale wa Jumuiya
ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa
Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na waangalizi
kutoka nchi za Marekani na Uingereza.
Anasema kwamba kitendo cha kupindua maamuzi ya Wazanzibari kupitia
uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kilifanywa kwa baraka zote za
aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati huo, Jakaya Kikwete.
Anasema hakuna mtu mbaya kwa Zanzibar na Wazanzibari kama Jakaya
Kikwete. Kwa hivyo, anasema kudai kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano
hana mamlaka kuliingilia kati suala la Zanzibar ni unafiki wa hali ya
juu.
Maalim Seif ameweka msimamo wa CUF hadharani kwamba uchaguzi wa
marudio si halali na si ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi uliopo huku
akisisitiza kwamba uchaguzi ulishafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.
Amewaeleza kwa kina yaliyojiri katika vikao 9 vya mazungumzo kati
yake na Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Marais wastaafu na kuweka wazi
kwamba mazungumzo hayo hayakufanikiwa kwa sababu Dk. Shein hana nia
njema na si mkweli. Amesema Dk. Shein ni mtu anayeamini kutawala kwa
mabavu na matumizi ya nguvu na asiyejali wala kuheshimu Katiba.
Maalim Seif anawataka wana-CUF kutembea kifua mbele wakijua kwamba wao ndiyo WASHINDI HALALI wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
Amemalizia kwa kusisitiza tena kwamba msimamo wa CUF kama ulivyotangazwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa UKO PALE PALE!
0 comments:
Post a Comment