Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meneja
wa Mawasiliano TCRA Makao makuu Innocent Mungy akizungumza na
Wanahabari kuhusu zoezi la kuzifungia Simu Bandia na zitakazobainika
kutumia Namba za Usajili Bandia ifikapo June 16,2016 katika hafla
iliyofanyika ukumbi wa Zanzibar Ocean View mjini Zanzbar .
Baadhi
ya wandishi wa Habari waliofika katika Mkutano wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania TCTA unaohusu kuzifungia Simu Bandia ifikapo Juni
16 kwaka huu.
Naibu
Mkurugenzi, masuala ya watumiaji wa huduma za mawasiliano Thadayo Ringo
akimuanyesha mmoja wa wandishi namna ya kuweza kuijua simu Bandia.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 03.02.2016
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania TCRA imesema ifikapo June 16 mwaka huu
itavifungia Vifaa vya Mawasiliano vya Mkononi hususan Simu na Tableti
ambavyo vinatumia namba tambulishi Bandia.
Hatua hiyo ni miongoni mwa njia muhimu za kudhibiti wizi wa Simu na kuhimiza utii wa sheria nchini.
Hayo
yameelezwa na Meneja wa Mawasiliano Makao makuu Innocent Mungy alipokuwa
akizungumza na Wanahabari kuhusu kuzifungia Simu hizo katika ukumbi wa
Zanzibar Ocean View mjini Zanzbar.
Amesema
kifungu cha 84 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta
(EPOCA) ya mwaka 2010 kinataka kuwepo kwa Mfumo wa rajisi ya namba za
utambulisho wa Vifaa vya mawasiliano na inawataka watoa huduma za
mawasiliano yanayotumia vifaa vya mikononi kuweka mfumo wa kudumu wa
kumbukumbu za namba Tambulishi ya vifaa hivyo.
Mungy
amefahamisha kuwa mfumo huo wa kielektroniki ambao utahifadhi kumbukumbu
za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi una lengo la
kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika, kupotea
au ambavyo havikidhi viwango vya matumizi katika soko la Mawasiliano.
Aidha
amesema kuwa vifaa vyote vya mawasiliano ambavyo Vimeibiwa, kupotea au
visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaweza
kufanya kazi kwenye mitandao ya mawasiliano kuanzia Juni 20.
“Mfumo
huu sio mgeni kwa nchi za wenzetu hata Kenya wanatumia na tayari
wameshazifungia Simu Feki kwa hiyo kabla sisi kuzifungia tunalazimika
kuwaelewesha Wananchi kabla ya hiyo June 16 Mwaka huu” amesema Mungy.
Kwa
upande wake Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa huduma za
mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akielezea faida za huduma hiyo amesema
iwapo mtu amepoteza au kuibiwa Simu ya mkononi na akatoa taarifa kwa
Mtoa huduama, simu hiyo itafungiwa isiweze kutumika kwenye mtandao
mwingine wowote nchini.
Aidha
ametoa wito kwa wananchi mara tu wanapopoteza simu zao za mkononi kwenda
kutoa taarifa kituo cha Polisi ambapo atapewa namba ya kumbukumbu ya
taarifa ya kituo maarufu kama RB kama utibitisho wa umiliki wa simu
iliyopotea.
Akizungumzia
juu ya hatua za kuchukua iwapo Mtu atakuwa na simu Bandia isiyokidhi
viwango amesema itamlazimu mtu anunue simu nyingine kwa gharama yake.
Akielezea
namna ya kutambua namba Tambulishi Ringo amesema mtumiaji atatakiwa
aandike Tarakimu *#06# kwa kutumia Simu yake ambapo kutaonekana namba
ndefu na hivyo namba hizo kutakiwa azitume kwa njia ya ujumbe mfupi
kwenda namba “15090” ambapo atapokea ujumbe kufahamisha uhalisia wa simu
yake.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa sasa wapo Zanzibar kutoa elimu kupitia
vyombo vya habari kwa ajili ya kuwajengea uelewa wananchi kutambua
iwapo Simu zao hazitumii namba tambulishi Bandia kabla ya kuzifungia
ifikapo June 16 2016.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.
0 comments:
Post a Comment