Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA
cha Mapinduzi Zanzibar kimesema hakitowavumilia baadhi ya watu
wachache wanaotumia hati bandia kupora mali za chama hicho kwa
makusudi.
Hayo
ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar katika mwendelezo wa ziara
ya kuhakiki na kukagua mali za Chama na Jumuiya zake huko katika jengo
la mradi wa UVCCM Zanzibar uliopo darajani Unguja.
Vuai
alieleza kwamba CCM itawachulilia hatua za kisheria baadhi ya watu
watakaobainika kupora mali zake, kwani watakuwa sio watu wema wanaotaka
chama hicho kisonge mbele kimaendeleo.
Alisema
CCM italinda mali zake kwa gharama yoyote ili kuhakikisha hazihujumiwi
na baadhi ya watu wachache wasiokitakia mema chama hicho.
Alieleza kwamba chama hicho kitapambana na watu wanaohujumu mali za chama hata kama watakuwa wanatoka ndani ya chama hicho.
Aliwataka
viongozi wa CCM na jumuiya zake kuhakikisha wanalinda na kusimamia
vizuri mali za chama hicho ili zibakie kuwa katika ulinzi wa kudumu.
Vuai
alisema bila ya kuweka mikakati endelevu ya kulinda rasilimali za chama
hicho zitapotea kidogo kidogo na kumalizika kabisa na kumilikiwa na
watu wachache wasiopenda kuona CCM inapata maendeleo.
“
Mali hizi hazikubatikana kirahisi kama ambavyo baadhi ya watu
wanaojimilikisha rasilimali zetu kinyume na sheria wanavyodhani, mimi
nawambia waache tabia hiyo na ambao tayari wameshachukua wazirejeshe
mapema vinginevyo watapambana na mkono wa sheria.’, alisema Vuai.
Naye
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Abdulghafar Idrissa alisema
mradi huo unaosimamiwa na umoja huo kwa kushirikiana na mwekezaji
mzalendo wa Kampuni ya Mishely Co. LTD unaendelea vizuri licha ya kuwepo
kwa changamoto za kiutendaji zinazokwamisha mradi huo kutokamilika kwa
wakati.
Alisema
endapo Chama na jumuiya kwa kushirikiana na mwekezaji huyo watakaa
pamoja kwa kujadiliana ili wapate maamuzi ya pamoja yatakayosaidia
kutatua changamoto hizo kwa haraka.
Idrissa alikiahidi chama hicho kuendelea kulinda mali za umoja huo ili zisiingie katika mikono ya watu wenye tabia za kitapeli.
Wakati
huo huo alitembelea eneo la chama hicho lililopo makontena Vikokotoni
Zanzibar , alisema CCM inakusudia kuanzisha mradi wa kujenga majengo
ya kisasa yatakayojumuisha maduka na ofisi ili kuwatengenezea mazingira
mazuri wafanyabiasha wa maeneo hayo.
Aliwasihi
wafanyabiashara wa eneo hilo kutoa ushirikiano wakati chama hicho
kitakapohitaji eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kisasa.
Alisema
lengo la CCM ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha Zanzibar
inakuwa na majengo ya kisasa na yenye hadhi yatakayowavutia
wafanyabiashara wakubwa kuwekeza katika eneo hilo .
Naibu
Katibu Mkuu huyo alisema muonekano wa eneo hilo linalofanyiwa biashara
kwa sasa umepitwa na wakati unahitaji uimarishwaji wa miundo mbinu
unaoendana na mazingira ya sasa kibiashara.
Naye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Vikokotoni Zanzibar Juma
Said, alikipongeza Chama cha Mapinduzi kwa kuendelea kushirikiana
vizuri na wafanyabiashara wa eneo hilo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa
Chama hicho.
0 comments:
Post a Comment