Kushoto Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu wa Rais anaeshughulikia
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipata Maelezo toka kwa Dkt. Mohammed
Maalim Mtaalam wa Maabara ya Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM
..iliyopo Zanzibar, moja wapo ya taasisi ya Muungano ililopo chini ya Wizara ya
Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania. Naibu Waziri Mpina Yupo Mjini Zanzibar katika ziara ya kikazi.
Katika Picha ya pamoja aliyekaa kati kati Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina pamoja na watumishi
wa Taasisi ya ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, iliyopo Buyu katika wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya
mji mkongwe wa Zanzibar.
Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kati kati ni Dkt. Yohana Shebule muhadhiri wa ya Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, na Makamu Mkurugenzi wa Taasisi
hiyo Profesa Mtolela wakitembea kukagua jengo jipya la taasisi hiyo lililopo
Buyu, nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina, pamoja na ujumbe wake
wakisikiliza taarifa na changamoto za jengo jipya la za Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, toka kwa dkt.Yohana Shebuda hayupo pichani, wakati wa kukagua jingo
hilo pamoja na kuzungumza na watumishi wa taasisi hiyo
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina kushoto Pamoja na ujumbe wake.wakiendelea kukagua jengo la
Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi hiyo lililopo Buyu, nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar. (Picha
na Habari zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)
Naibu waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luahaga Mpina Ametoa
wito kwa taasisi za Muungano zinazofanya tafiti za kisayansi, kufanya tafiti
hizo ziwe na tija kwa Serikali na Umma.
Mpina aliyassema hayo, alipotembelea taasisi ya Muungano ya
Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM ..iliyopo katika Wilaya ya Magharibi B
nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar,
iliyopo chini ya Wizara ya Wizara ya
Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Baada ya Kukagua jengo
jipya la taasisi hilo ambalo halijaanza kutumika ikidaiwa ni kutokana na
changamoto mbalimbali pamoja na ukosefu wa samani, Naibu Waziri Mpina
aliishauri tafiti za taasisi hiyo ziwe zenye malengo ya kusaidia watanzia
wanaoishi katika ukanda wa pwani ili kuwawezesha kusaidia kuinua uchumi wao na
kuongeza pato la taifa.
Aidha, Mpina aliongeza kwa kusema kuwa anategemea tafiti
zinazofanywa na taasisi hiyo zitoe muongozo kwa serikali na namana ambavyo nchi
inavyoweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. “Hakikisheni
serikali inapata taarifa zenu ili ziweke kutumika, mpo kimya sana na
hamsikiki.” Alisisitiza Mpina.
Kwa upande mwingine taasisi hiyo imekuwa pia ikitoa nafasi
kwa wanafunzi wageni toka katika nchi mbali mbali duniani kuja kujifunza na
kufanya tafiti juu ya viumbe hai waishio baharini aina ya
Pomboo (Dolphin)ili kuweza kufahamu mazingira na tabia za ndani za
viumbe hao na kubadilishana uwezo na kuongeza kipato kwa taasisi hiyo kupitia
malipo ya mafunzo hayo maalum.
Naibu Waziri Mpina pia, alitoa Pongezi kwa
taasisi hiyo kuwa na jengo zuri pamoja na changamoto wanazokabilana nazo na
kuwashauri wahamie na kuanza kulitumia jengo hilo. Ziara ya Naibu Waziri Mpina
Mjini Zanzibar pamoja na kumuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano
Mhe.Samia Suluhu Hassan katika siku ya Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja,
inahusisha pia kutembelea baadhi ya taasisi za muungano mjini humo.



0 comments:
Post a Comment