Mabinti Mapacha Sabra na Sabrina Hassan wa shule ya sekondari
makunduchi wakitumbuiza kwa utenzi kwa meza kuu haipo pichani, wakati wa
mkutano wa Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina Hayupo pichani, kijijini Kizimkazi wakati wa siku ya kizimkazi ambapo Naibu waziri Mpina
alimuwakilisha Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyewahi kuwa mbunge wa
jimbo la makunduchi.
Aliyesimama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na baadhi yaViongozi mbali mbali wa jimbo la
Makunduchi mkoa wa kusini Unguja, akizungumza na wanachi (hawapo pichani) wa
jimbo hilo katika kijiji cha kizimkazi .katika siku ya kizimkazi maarufu kama
kizimkazi day, alipomuwakilisha mhe. Mkamu wa Rais Mama Samia Suhulu Hassan
aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Aliyesimama katikati Mkurugenzi wa Kampuni ya Blue Spot Bw
Buhet Juma ya Mjini Unguja inayotengeneza nishati ya mkaa ambayo ni rafiki kwa
mazingira akimuonyesha Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira aliyesimama kushoto, ambavyo
nishati hiyo inavoengenezwa.
Naibu Waziri Mpina
aliyesimama kati kati akishika chembe za malighafi inayotengeneza nishati ya
mkaa rafiki kwa mazingira, alipotembelea kiwanda kidogo cha Ble Spot Mjini
Unguja kumwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aliyekaa katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Ris
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika Picha ya Pamoja na baadhi ya
watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Raisi, Pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya
kutengeza nishati ya Mkaa rafiki wa mazingira, katika kiwanda cha Blue Spot.
(Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)
Wakazi wa kijiji cha Kizimkazi kilichopo katika jimbo la Makunduchi Mkoa wa kusini unguja,
kimekuwa na utaratibu wa kuadhimisha siku ya kizimkazi, maarufu kama kizimkazi day ambayo hufanyika kila
mwaka mwezi wa nane.
Siku hiyo maarufu katika kijiji hicho ambayo imeanzishwa na
aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo la Makunduchi mhe.Samia Suluhu Hassan ambae
sasa ni Makamu wa Rais wa JAmuhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa
ikiadhimishwa kijijini hapo kwa namna ya kipekee ya burudani, mashairi na
michezo mbali mbali ambapo pia wana kizimkazi wamekuwa wakipata nafasi ya
kuainisha changamoto mbali mbali zinazo wakabili kagtika kijiji hicho.
Akimuwalisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu
waziri Ofisi ya Makamu wa RAis Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina amehaidi
kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi wa kijiji hicho
kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Makunduchi mhe. Haruna Suleiman ambae
pia ni Waziri wa Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuchangia mifuko 100 ya simenti na mabati 100, na
matofali 2000 ya kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vimeanishwa kuwa
moja ya changamoto kijijini hapo.
Aidha, amehaidi wana kizimkazi kuwa kwa kushirikiana na
mbunge na uongozi wa serikali uwanja wa mpira ambao umekuwa ukihitaji matengezo
nao utaanza kusawazishwa kwa ajili ya michezo kijijini hapo.
Wana Kizimkazi wamebainisha kukabiliana na changamoto
itokanayo na mapato na matumizi ya rasilimali ya bahari, pamoja na kupungua kwa
nishati ya umeme kutokana na ongezeko la mahitaji litokanalo na mji huo
kupanuka.
Kwa upande mwingine Naibu Waziri Mpina Pia alimuwailisha
Makamo wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kampuni inayotengeneza
nishati ya mkaa rafiki wa mazingira inayotumia malighafi itoknayo na taka za
maganda ya miwa na makarati na
kuwapongeza kwa jitihada kubwa za utunzaji wa mazingira kwa kutokukata miti
ovyo na ubunifu wa nishati hiyo.
Ziara ya naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar ni Sehemu ya
utekelezaji wa majukumu yake katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Pamoja na
kumuwakilisha Mhe, Makamu wa Rais katika siku maalum ya Kizimkazi. Kizimkazi
Day.






0 comments:
Post a Comment