Anayeongea kwa vitendo ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa menejimenti ya Bank Kuu tawi la Zanzibar mara baada ya kutembelea taasisi hiyo ya muungano mjini Unguja.
Bi Safia Hashim, Mtengenezaji na Muuzaji wa mapambo na sabuni zitokanazo na zao la mwani, mdau anayefadhiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia COSTECH taasisi ya muungano iliyopo chini ya wizara ya Elimu na Sayansi ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania tawi la Zanzibar, akimuelezea Naibu Waziri Mpina faida na matumizi ya zao la mwani na kuonyesha bidhaa zake katika maonyesho yaliyoandaliwa na taasisi hiyo mjini Unguja wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Mpina.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na baadhi watumishi wa tume ya sayansi tawi la
Zanzibar. COSTECH alipotembelea
taasisi hiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar. (Picha zote na Habari na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)
Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais anayeshughulikia Muungano
na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameendelea na ziara yake Mjini Ugunja na
kutembelea taasisi za Muungano ikiwa ni pamoja na Bank kuu ya Tanzania tawi la
Zanzibar na Tume ya Sayansi na Teknolojia iliyopo chini ya Wizara ya Elimu na
Sayansi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya uwasilishwaji wa taarifa fupi ya utekelezaji wa Bank
kuu tawi la Zanzibar, na Naibu Gavana wa Bank hiyo Dkt. Natu Mwamba, Bw. Mansour
Abdalla Meneja wa fedha na
utawala wa Bank hiyo tawi la Zanzibar alieleza kuwa dhana ya ajira kwa
watumishi wa Bank hiyo kwa ni ya upendeleo na kujuana haina ukweli wowote
kutokana na sababu kuwa taratibu ajira za Bank hiyo zimewekwa pamoja katika
makao makuu ya Bank hiyo jijini Dar es Salaam na huwa nafasi za kazi hutangazwa
katika magazeti na wananchi wenye vigezo kupata kazi.
“wananchi wajenge tabia ya kusoma magazeti hasa kwa wale
wanaotafuta ajira katika bank hii kwani kazi za hapa huwa zinatangazwa huko na
bank inatoa ajira bila upendeleo na kwa upande wa Zanzibar asilimia 48% ya
watumishi ni wazanzibari na asilimia inayobakia ni ya upande wa pili wa
Muunano.” Alisisitiza Bw. Mansour.
Akitolea ufafanunuzi suala la mgawo wa asilimia 4.5% ya
mapato ya Bank hiyo kwa Zanzibar kama sehemu ya Muungano, Mkurugenzi wa Fedha
wa Bank hiyo Tawi la Zanzibar bw. Jamhuri Ngelime alisema kuwa hana Jibu la
moja kwa moja kuhusu mgao huo ila serikali hizi mbili za muungano zilikubaliana
kuwa asilimia 45% ya faida ya Mapato yote ya Bank hiyo nchini igawiwe kwa
Zanzibar, na hivyo sheria ndiyo inavyosema.
Kwa Upande wake Naibu Waziri Mpina, aliitaka Bank hiyo
kufanya bidii ili kuhakikisha inafikia malengo ambayo serikali imejiwekea, na
kuishauri bank hiyo kuongeza huduma zake za ki bank hasa kwa upande wa Pemba na
kuweka masharti nafuu kwa wafanya biashara wenye ma bank, ili kuweza kutoa
huduma hiyo na kuondoa gape ya
kifedha iliyopo kati ya Unguja na Pemba.
Wakati Huo Huo,
Naibu Waziri Mpina aliitembelea Tume ya Sayansi na Teknolojia
tawi la Zanzibar COSTECH na katika majadiliano na watumishi wa tume hiyo Naibu
Wazri Mpina alisema kuwa tafiti za kisayansi ni muhimu sana kwa nchi yoyote duniani kuendelea, nchi haiwezi
kuingia kwenye Biashara ya Gas na oil bila wana sayansi kufanya tafiti zao.
Na kupongeza mchango wa taasisi hiyo katika jamii, ikiwa ni
pamoja na kufadhili wanachuo wanasansi mbali mbali nchini.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mjini Unguja ilihusisha
kutembelea taasisi za Muungano, Kumuwakilisha Mhe. Makamu wa Raisi wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika siku ya Kizimkazi
alipozaliwa Makamu wa Rais, Pamoja na Kutembelea Ofisi zake zilizopo Tunguu nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment