Home » » NDOTO ZA ZANZIBAR KUSHIRIKI MICHUANO YA CAF ZAFUTIKA, YAVULIWA UANACHAMA

NDOTO ZA ZANZIBAR KUSHIRIKI MICHUANO YA CAF ZAFUTIKA, YAVULIWA UANACHAMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefanya maamuzi ya kuwavua uanachama chama cha soka cha Zanzibar ikiwa ni miezi minne toka kipewe uanachama na CAF kutoka kwa Rais aliyepita Issa Hayatou.

Rais wa CAF Ahmad Ahmad (pichani) amesema Zanzibar walipewa uanachama kimakosa na kama sheria zingepitiwa vizuri wasingepewa uanachama.

“Walipewa uanachama bila kupitia vizuri kanuni ambazo ziko wazi na zinaeleza kila kitu, kama kanuni na sheria zingepitiwa kiufasaha wasingepewa uanachama”, alisema.

Sababu kubwa ambayo CAF wameivua uanachama Zanzibar ni kutokana na kisiwa hicho kuwa ndani ya Tanzania ambao nao ni wanachama wa CAF.

“Jina la nchi linatokana na jina linaloandikwa katika umoja wa mataifa UN na Zanzibar katika umoja huo inafahamika ipo ndani ya nchi iitwayo Tanzania ambao ni wanachama wa CAF” alisema Ahmad.

Hilo ni pigo kubwa kwa Wazanzibari kwani wakati huu walikuwa wakipambana kupata uanachama wa FIFA ambao wameukosa na wa CAF nao pia wamekosa.

Kwa maana hiyo ndoto ya kisiwa cha Zanzibar kushiriki michuano ya CAF kama mwanachama zimekufa rasmi na sasa watakuwa wakishiriki michuano hiyo kama Tanzania (Zanzibar na Tanzania bara).

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa