Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwakilishi
wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa na Mbunge wa
Jimbo hilo Mhe Khalafa Salum Suleima wakishiriki katika ujenzi wa Taifa
wa kujenga Soko la Samaki katika ufukwe wa pwani ya Kijiji cha Tindini
Unguja Ukuu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja, wakikata majengo ya kuezekea
bati katika soko hilo. Pia wamekabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi huo
ili kutowa mazingira mazuri ya Soko hilo wakati wa kufanya mnada wa
samaki kwa wavuvi wanaporudi baharini kuvua.
Wananchi
wa Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu wakishirikiana na Mbunge wao na
Mwakilishi katika ujenzi wa Taifa wa Soko la Samaki katika ufukwe wa
Bahari ya Unguja Ukuu Zanzibar.
Mbunge
nas Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said ma
Mhe Khalifa Salum Suleiman wakikabidhi mabati kwa Katibu Mkuu wa CCM
Mkoa wa Kusini Unguja Bi. Sauda Ramadhani, hafla hiyo ya makabidhiano ya
Mabati hayo na miti yamefanyika katika viwanja vya Soko hilo Kijiji cha
Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini.
Wananchi
wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki
Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa
kijiji hicho kuuzia samaki wao..
Wananchi
wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki
Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa
kijiji hicho kuuzia samaki wao
Kiongozi
wa Kijiji cha Tindini akitowa maelezo ya ujenzi wa Soko hilo la Samaki
katika ufukwe wa bahari yao litakalotowa huduma ya kuuzia samaki kwa
wavuvi katika soko la mnada.
Mwakilishi
wa Jimbo las Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kumalizia
ujenzi wa Soko la Samaki katika kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya
Kati Unguja na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitumia soko hilo kwa
shughuli zao za biashara ya samaki na minada kwa wavuvi wanaorudi
bahari kuvua.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo kwa Wananchi wa Jimbo lake.
Katibu
wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Bi Sauda Ramadhani
akizungumza wakati wa hafla hiyo ujenzi wa taifa na kukabidhi mabati na
vifaa vya ujenzi wa Soko la Samaki katika Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu
Wilaya ya Kati Unguja.
Wananchi
na wavuvi wa kijiji cha Tindini Unguja Ukuu wakimsikiliza mgeni rasmin
wakati wa hafla hiyo ya ujenzi wa Taifa na kukabidhi mabati kwa ajili ya
kumalizia ujenzi wa Soko hilo.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge na
Mwakilishi na Wananchi wa Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu baada yas hafla
hiyo.
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspots.com
0 comments:
Post a Comment