Na. MWAJUMA JUMA-ZANZIBAR
Mabadiliko ya kweli katika mifumo ya kanuni na sheria yatategemea kwa kiasi gani wazee wataweza kuyachukulia kuhakikisha inawapeleka wanapotaka, imeelezwa.
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Kusaidia Wazee, Smart Daniel aliyaeleza hayo katika mafunzo ya siku tatu ya wazee kuhusu pensheni ya jamii, hali stahiki na namna ya kuzifikia programu na huduma za hifadhi ya jamii kwa wazee.
Hata hivyo, alisema Zanzibar imekuwa nchi ya mfano katika suala zima la kuwahifadhi wazee ikiwa ni pamoja na kuwapatia pensheni kila mwisho wa mwezi.
Alisema ingawa kiasi hicho ni kidogo, nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikiiga kupitia kwao.
“Jambo la msingi ni kujipanga na kuona kwa kiasi gani wazee hao wanakuwa na ushirikiano na Serikali kuona penye kasoro panarekebishwa,” alisema.
Hata hivyo alisema Serikali kuu imekuwa ikijitahidi lakini changamoto ipo kwa ngazi za chini.
Alisema ni jukumu la wazee kuona kila jambo ambalo wanataka wakae na kushauriana na baadaye taarifa ziweze kufikisha kunakohusika kinyume chake hawataweza kufikia malengo.
Alisema shirika lao limeamua kufanya Tanzania kuwa mwenyeji wa mouton Novemba ikiwa na lengo la kusherehekea nchi ndogo kama Zanzibar kufanya jambo kubwa kwa wazee wake
Chanzo Mtanzania
0 comments:
Post a Comment