Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
07.08.2017
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amesisitiza haja ya kuwaandaa viongozi wa
michezo hapa nchini watakaoendelea kuipa sifa Zanzibar katika sekta hiyo kama
ilivyokuwa hapo siku za nyuma.
Dk. Shein aliyasema hayo leo,
alipokutana na uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo pamoja
na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Michezo na Uongozi wa Baraa la Michezo katika
vikao vinavyoendelea Ikulu mjini Zanzibar.
Katika vikao vya leo, Dk.
Shein kwa nyakati tofauti alikutana na Uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii,
Utamaduni na Michezo, Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu
ya Uongozi wake, Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Michezo na uongozi wake
pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Kiswahili na uongozi wake.
Dk. Shein katika maelezo
yake alieleza kuwa hatua hiyo itapelekea kuwapata viongozi bora wa michezo
hatua ambayo itasaidia hata kupunguza migogoro inayotokea katika vyma na vilabu
vya michezo hapa nchini.
Aliongeza kuwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuona umuhimu wa suala hilo katika sekta ya michezo
katika chuo chake kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimeweza kuanzisha kada
inayohusiana na michezo ambayo hutoa mafunzo juu ya masuala yote ya michezo
ikiwemo uongozi.
Sambamba na hayo, Dk.
Shein alitoa pongezi kwa uongozi na Bodi
hiyo ya Baraza la Michezo kwa kuendeleza vyema juhudi za ujenzi wa viwanja vya
michezo katika Wilaya zote hapa nchini ambapo kwa upande wa Wilaya ya Kusini
kiwanja cha Kitogani kiko ukingoni kumaliza ujenzi wake.
Nae Waziri wa Habari,
Utalii, Utamaduni na Michezo Rashidi Ali Juma alitoa pongezi zake kwa Rais Dk.
Shein kwa juhudi zake alizozianza tokea kuwa Rais wa Zanzibar katika
kuhakikisha sekta ya michezo inapata mafanikio na kuimarika zaidi.
Waziri Rashid alieleza
kuwa umefika wakati vilabu viweze kuwezeshwa na kuahidi kuwa uongozi wa Wizara yake
utaandaa mipango kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya kuendeshea michezo
hatua ambayo itawavutia na hata wafadhili watakaokuja kuunga mkono sekta ya
michezo hapa nchini.
Alieleza kuwa wananchi
walio wengi hapa Zanzibar wanapenda michezo na wako tayari kuchangia michezo
jambo linalotakiwa ni kuweka mikakati katika kuhakikisha sekta hiyo inaimarika ikiwa
ni pamoja na kutoa viingilio katika viwanja vya michezo kwa wingi na kutolea
mfano kiwanja cha Gombani Pemba jinsi wananchi wapenda michezo wanavyojaa kwa
wingi.
Nae Katibu Mkuu Kiongozi
na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee kwa upande wake alisisitiza
haja ya kuwepo viongozi makini katika sekta ya michezo
Aidha, aliongeza kuwa
michezo ni gharama hivyo ni lazima kuwepo vyanzo vya fedha kwa ajili ya
kugharamia michezo.
Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar Said Hassan alieleza haja ya kuibua vipaji kwenye michezo sambamba na
kupata usimamizi mzuri huku akieleza haja ya kuwepo kwa vituo vya kuendeleza
michezo.
Mapema, Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo Zanzibar (BTMZ), Sharifa Khamis Salim alieleza kuwa Baraza
kwa kushirikiana na Afisi ya Mrajis linatioa muongozo juu ya mambo mbali mbali
kwa Vyama na Vilabu vya michezo na kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa
kanuni za Usajili wa vyama vya michezo za mwaka 2014.
Aidha, akieleza miongoni
mwa mafanikio Mwenyekiti huyo alisema kuwa Chama cha Viziwi kimepata uwanachama
wa Shirikisho la mpira wa miguu la Afrika ya Mashariki la viziwi (DEFA) na Rais
wake anatoka Zanzibar.Pia, Zanzibar ni mwanachama wa Shirikisho la Kimataifa la
Viziwi la mpira wa miguu (DIFA).
Wakati
huo huo,
Dk. Shein alikutana na uongozi wa Wizara hiyo pamoja na Bodi yake ya
Wakurugenzi ya Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu pamoja na uongozi wa Baraza
hilo alieleza haja ya kuwatunza wasanii wa zamani na kuwaenzi wale wa hivi
sasa.
Pia, Dk. Shein alieleza
azma ya Serikali ya kuitengeza studio mpya iliyopo Rahaleo kwa lengo la
kuwainua vijana katika maisha yao huku akieleza haja kwa Wizara kufanya
utaratibu wa kuwatunza wasanii wakiwemo waibaji, waigizaji na hata wapiga
vyombo.
Akieleza haja ya
kuimarisha utamaduni wa hapa nchini Dk. Shein alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa
kudhibiti mmongonyoko wa maadili hapa nchini.
Nae Mwenyekiti wa Baraza
hilo, Bi Mariama Hamdani alieleza mafanikio na changamoto za Baraza hilo
Aidha, aliongeza kuwa
Baraza limeweza kufanya ukaguzi wa kazi za sanaa 30 za filamu na 136 za muziki
na kufanya jumla ya kazi za sanaa zilizokaguliwa kufikia 172 na kati ya hizo 5
zilizuiliwa kuoneshwa hadharani na kazi 7zimezuiliwa kuoneshwa hadharani na
hata faragha kutokana na kwenda kinyume na maadili ya Zanzibar.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
0 comments:
Post a Comment