Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Habiba Zarali, Pemba
OFISA Mdhamini Wizara ya Ardhi,Maji ,Nishati na Mazingira Pemba, Juma Bakar Alawi, amesema utamaduni ulioanzishwa na Wanafunzi wa upandaji miti maskulini, kutasaidia kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali za kimazingira zilizopo katika maeneo yao wanayojifunzia pamoja na maeneo wanayoishi.
Kauli hiyo aliitowa katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa Skuli
za Sekondari ya Kangani na Skuli ya msingi Makombeni Wilaya ya
Mkoani Pemba, ambazo ni miongoni mwa Skuli zilizofanya vizuri katika
mradi wa mazingira maskulini “ECO SCHOOLS”inayofadhiliwa na Zayadesa
na kutekelezwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Alisema
mradi huo ni miongoni mwa hatuwa zinazochukuliwa katika kutekeleza kwa
vitendo malengo endelevu ya sasa ya dunia, pamoja na utekelezaji wa
lengo ambalo linahusika na utowaji wa elimu stahiki ya maendeleo
endelevu ya rasilimali hiyo.
Alifahamisha udumishaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti ni
hazina kubwa iliyotoka kwa wazee ambao waliweza kuilinda na kuiendeleza
hadi kufikia leo hii, sasa basi ni jukumu la vizazi vya sasa kuona
umuhimu
huo ambao utasaidia matumizi endelevu ya rasilimali hiyo, ili vizazi vijavyo navyo viweze kufaidika.
“Wanafunzi
mradi huu ni fursa kwenu wala musione kama ni utumwa kwani upandaji
wa miti ni usafi wa mazingira ambao hata dini ya kiislamu imehimiza na
kusema muislamu ni usafi”alisema.
Alifahamisha
ili nusra iweze kupatikana kwa kuepusha mmong’onyoko ,maporomoko na
maji ya bahari kupanda juu ni jukumu la jamii kuwa mstari wa mbele
kupanda miti kwa wingi, sambamba na kupeana elimu ambayo itasaidia
kuwashajihisha wale ambao bado uwelewa wao ni mdogo.
“Nyinyi
wanafunzi ambao tayari mumeshapata mafunzo ya utunzaji wa mazingira
kupitia Skuli zenu, sasa mutowe elimu majumbani ili nako jamii iweze
kuelewa umuhimu wa utunzaji wa mazingira “alisema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa ECO SCHOOLS Zanzibar , Abdul-Aziz Mohammed
Iddi , akitowa taarifa kuhusu mradi huo, alisema utawapatia nchi
wanachama fursa za kuitambuwa ,kuziendeleza na kuzitekeleza njia ,mbinu
na dhana za kukabiliana na changamoto endelevu za kimazingira kama vile
mabadiliko ya tabia nchi ,matumizi ya rasilimali ,majanga ya kimaumbile
,udhibiti wa taka na uharibifu wa matumbawe.
Alisema
Skuli kupitia mradi huo zina fursa kufanya kazi kwa pamoja katika
kukabiliana na matatizo yanayozikabili nchi zinazoendelea za Visiwa
vidogo vidogo kwa kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa kwa kupata
zawadi mbalimbali.
“Kwa
kuwa mradi huu ni endelevu mwelekeo wake basi ni ushiriki wa
wote ambapo uhamisho au kustafu kwa mwalimu au kumaliza Skuli kwa baadhi
ya wanafunzi hakuwezi kuathiri uwepo wake”, alisema.
Mapema wakisoma risala ya eco program, Skuli ya Kangani walisema
baada ya kuingia katika mradi huo wamepata mwamko mpya juu ya uhifadhi
wa mazingira ,kuimarisha usafi wa Skuli pamoja na jamii zao ,kujifunza
mambo mbalimbali ya asili kama vile kupiga kumba na madawa ya asili waliokuwa wakitumia wazee wao.
Walisema
hadi sasa wanahifadhi mazingira ya bahari kwa lengo la kuzuwia
mmong’onyoko wa ardhi na kuzuwia maji chumvi kuingia katika mashamba na
makaazi ya watu.
Jumla
ya Skuli 30 teule za Serikali na za binafsi kutoka
Zanzibar zinatekelezwa na mradi huo, ambapo kwa Unguja ni 21 na Pemba ni
9, na Skuli 12 ikiwemo ya Sekondari Kangani na msingi Makombeni
zimeweza kufikia viwango vya kujipatia tunzo mbalimbali zikiwemo Ngao
za Shaba na za Dhahabu.
0 comments:
Post a Comment