Mkuu wa Wilaya ya Wete
Omar Khamis Othman amesikitishwa na taarifa za matokeo ya chanjo ya watoto
katika Wilaya hiyo na kuutaka uongozi wa Wizara ya Afya Wilayani humo kuandaa
mipango itakayofanikisha kupata mafanikio katika zoezi la chanzo mwaka huu .
Akizundua wiki ya chanjo ambayo huadhimishwa na nchi
za Afrika kuanzia april 22 hadi april 27 , amesema kuwa kiwango cha matokeo
ya chanjo kwa mwaka jana si mazuri na kwamba Wizara inatakiwa kuongeza
uhamasishaji kwa wananchi ili kuwapeleka watoto kupata chanjo .
Amesema katika mwaka jana Wilaya ya Wete ilifanikiwa kutoa
chanjo wa watoto asilimia 85 ikiwa ni pungufu ya asilimia kumi yaa maelngo
yaliyowekwa na shirika la kuhudumia watoto la ulimwenguni UNECEF
Aidha amewataka watendaji wa Wizara Afya Wilayani humo
kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa msitari wa mbele kuwapeleka watoto zao pamoja na
kuwahimiza ndugu zao wa karibu kwenda kupatiwa chanjo hiyo .
Kwa upande wake Afisa wa Afya Wilaya ya Wete Dk Ali Rashid
amesema kuwa pamoja na kuadhimisha Wiku ya chanjo Afrika lakini huduma hizo
zinaendelea kitolewa katika Hospitali na vituo vya afya katika Wilaya hiyo.
Amesema kuwa katika Wilaya ya Wete kuna vituo 19 vinavyotoa
huduma ya chanjo na wanaimani ya kupata mafanikio katika zoezi la chanjo
kutokana na jamii kuhamasika kutokana na elimu inayotolewa na watendaji wa
Wizara paamoja na viongozi wa kamati za afya za shehia .
Maadhimisho ya wiki ya chanjo Barani Afrika yalianza
kuadhimishwa mwaka 1980 ambapo Serikali ya Mapinduzi iliridhia maadhimisho
baada ya kuona kuwa watoto wengi wanapotesha maisha .
0 comments:
Post a Comment