Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na
Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali S S Othman,
alipofika ofisini kwake Migombani.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na
Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali S S Othman,
alipofika ofisini kwake Migombani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar,
Fatma Abdulhabib Ferej, akizungumza na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki
Zanzibar, Brigedia Jenerali S S Othman, alipofika ofisini kwake
Migombani.
Picha na Salmin Said, OMKR
Picha na Salmin Said, OMKR
Na Hassan Haamd
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amevitaka
vyombo vya ulinzi nchini kusimamia vyema majukumu yake ili kuhakikisha
kuwa bahari na mipaka ya nchi inakuwa salama.
Amesema Zanzibar ikiwa nchi ya visiwa, inakabiliwa na changamoto moto
nyingi za kiulinzi na usalama kuhakikisha kuwa magaidi hawaingii nchini,
sambamba na kukabiliana na vitendo vya uharamia na usafirishaji wa dawa
za kulevya.
Maalim
Seif ameeleza hayo ofisini kwake Migombani alipokuwa na mazungumzo na
Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali S S Othman.
Amesema katika siku za hivi karibuni kumekuwa ni tishio la vitendo vya
kigaidi katika Pembe ya Afrika, jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa ili
vitendo hivyo visije kuiathiri Zanzibar.
“Suala
la ulinzi halina mbadala, kitu cha msingi ni kwa vyombo vya ulinzi na
dola kushirikiana kuhakikisha kuwa nchi iko salama kwa maslahi ya
wananchi na taifa kwa ujumla”, alisisitiza Maalim Seif.
Kuhusu
vitendo vya uharamia vinavyofanywa katika bahari ya hindi, Maalim Seif
amesema vinaathiri shughuli za kibiashara na uchumi na vinastahiki
kupigwa vita kwa nguvu zote.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali S S
Othman, amesema suala la ulinzi ndio jukumu la msingi kwa vyombo vya
ulinzi, na kuahidi kushirikiana na vyombo vya dola na wananchi katika
kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi zaidi.
Jererali
Othman ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Zanzibar,
amesifu mashirikiano anayoyapata kutoka kwa viongozi wa nchi na
watendaji wengine katika kufanikisha jukumu hilo la kiulinzi.
Jererali Othman pia amekutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Fereji na kubadilishana mawazo juu ya
majumu ya ofisi hiyo.
Waziri
Fereji amesema katika kukabiliana na majukumu ya ofisi hiyo, wanahitaji
mashirikiano ya karibu na vyombo vya ulinzi katika kukabiliana na na
vitendo viovu vikiwemo udhalilishaji wa watu wenye ulemavu, uchafuzi wa
mazingira na matumizi ya dawa za kulevya.
Amevishauri vyombo vya ulinzi kujiimarisha zaidi ili kuweza kukabiliana
na makundi ya kihalifu yakiwemo yale yanayojihusisha na uchimbaji wa
mchanga kinyume na utaratibu.
“Ukweli
ni aibu kusema kuwa jeshi la polisi linashindwa kuwakamata wachimbaji
wa mchanga kwa sababu wana pamanga na marungu au mawe, wakija wakiamua
kuingia barabarani je mutawafanyaje?”, alihoji Waziri Fereji.
Kuhusu
UKIMWI, Waziri Fereji amesema licha ya kuwa kiwango cha maambukizi bado
ni chini ya asilimia moja, lakini athari kubwa inajitokeza kwa makundi
hatarishi likiwemo lile linalojihusisha na biashara haramu ya ukahaba.
0 comments:
Post a Comment