Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na waandishi wa
Habari wa vyombo mbali mbali nchini mara baada ya kuzindua mtambo wa
masafa ya mawasiliano Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa Mtambo maalum wa usimamizi wa masafa ya mawasiliano
Zanzibar hapo ofisi ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania iliyopo
Chukwani.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua Mtambo
maalum wa usimamizi wa masafa ya mawasiliano Zanzibar hapo ofisi ya
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania iliyopo Chukwani.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa SMT Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa akitoa melezo kwenye uzinduuzi wa Mtambo maalum wa usimamizi wa
masafa ya mawasiliano Zanzibar hapo ofisi ya Mamlaka ya mawasiliano
Tanzania iliyopo Chukwani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na waandishi wa
Habari wa vyombo mbali mbali nchini mara baada ya kuzindua mtambo wa
masafa ya mawasiliano Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
***************************************************
Makamu
Wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddialisema kasi ya
uwekezaji nchini inaweza kuongezeka mara dufu iwapo wananchi
watazingatia zaidi uimarishaji wa mazingira hasa katika mtandao wa
mawasiliano.
Alisema
wawekezaji wengi huvutika na hali ya mazingira safi yanayowashawishi
kupanua wigo wa mtandao huo ambao husaidia kupatikana kwa huduma zote za
msingi za mawasiliano kwa upande wa simu, posta na utangazaji.
Balozi
Seif alieleza hayo wakati akizindua mtambo maalum wa usimamizi wa
masafa ya mawasiliano Zanzibar hafla iliyofanyika katika Ofisi ya
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania { TCRA } iliyopo Chukwani nje kidogo ya
Maji wa Zanzibar.
Alisema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha mfuko wa mawasiliano kwa
wote ili kuunga mkono juhudi za wawekezaji binafsi na washirika wa
maendeleo katika ujenzi wa miundo mbinu ya mawasiliano kwenye maeneo ya
vijijini ambayo kibiashara bado hayajavutia wawekezaji.
Alieleza
kwamba Serikali imefanya hivyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 na Dira ya Taifa
ya Tanzania ya mwaka 2015.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewapongeza wawekezaji ambao uamuzi wao wa
kuwekeza hapa nchini hususan kwa visiwa vya Unguja na Pemba umesaidia
kukua kwa sekta ya mawasiliano na kuboresha njia za mawasiliano
Visiwani.
Balozi
Seif alisema ujio wa wawekezaji hao umesaidia kwa kiasi kikubwa
kupungua kwa gharama za mawasiliano ya simu na utangazaji ikiwa ni
pamoja na kuongeza pato la Taifa.
Ametoa
wito kwa wawekezaji zaidi kutumia fursa iliyopo nchini hususan
mazingira mazuri ya kisiasa na udhibiti bora wa kuwekeza kwenye ujenzi
wa miundo mbinu ya mawasiliano hapa Nchini.
Akizungumzia
utekelezaji wa uamuzi wa shiria la umoja wa Mataifa la mawasiliano ya
simu { ITU } wa kubadilisha teknolojia ya utangazaji wa Televisheni
kutoka analogi kwenda Digitali uliofikiwa na mwaka 2006 hadi 2015
Balozi Seif alisemaq Taasisi zinazohusika lazima zihakikishe watumiaji
wa huduma hizo hawaathiriki.
Balozi
Seif alizikumbhusha Taasisi hizo kufanya ukaguzi maalum wa kitaalamu
kwenye maabara na kuidhinisha viwango vyake kwa ving’amuzi
vinavyoingizwa hapa Nchini.
Alifahamisha
kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na juhudi za
kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi kwa ving’amuzi na Televisheni za
Digitali ili wananchi wenye kipato cha kawaida wamudu kuvinunua.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameishukuru mamlaka ya mawasiliano kwa
kufikia uamuzi wa kuweka mtambo maalum wa kusimamia masafa ya
mawasiliano Zanzibar.
Alisema
hatua hiyo ni busara ambayo itaiwezesha Zanzibar kudhibiti matmizi
mazuri ya masafa pamoja na huduma za mawasiliano kwa wananchi.
“
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefarajika kwa kutimiza wajibu wenu
na kuhakikisha kuwa Zanzibar pia inakuwa na uwezo wa kusimamia masafa
muda wote bila ya kusubiri mtandao kama huo kutoka Tanzania Bara “.
Alisisitiza Balozi Seif.
“ Nafurahi kuona Tanzania hivi sasa inajipanga kwenda kisasa zaidi “. Alifafanua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Akitoa
Taarifa fupi ya mtambo wa usimamizi wa masafa ya mawasiliano hapa
Zanzibar Mkurugenzi Mkuu bwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania { TCRA }
Profesa John Nkoma alisema maslahi ya watumiaji wa mawasiliano nchini
yanapaswa kulindwa wakati wote.
Profesa
Nkomo alisema Masafa ndio rasilmali katika Nyanja za mawasiliano hivyo
juhudi za kuendeshwa kitaalamu ni la msingi hasa ikizingatiwa ushindani
mkubwa uliopo hivi sasa wa sekta ya mawasiliano miongoni mwa makampuni
tofauti ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi
mkuu huyo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania aliihakikisha Jamii kwamba
mtambo huo utakuwa ukitoa huduma kwa ufanisi na kuboresha mawasiliano
kwa wananchi walio wengi Nchini.
Mapema
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamuhuri
yua Muungano wa Tanzania Profesa Makame Mnyaa Mbarawa alisema Wizara
hiyo iko mbioni kutunga sheria mbali mbali ili kuleta ufanisi zaidi
katika upatikanaji wa huduma bora za mawasiliano.
Profesa
Mbarawa alisema hatua hiyo imekuja kufuatia sekta ya mawasiliano
duniani kuendelea kukua na kubadilika kwa haraka kiteknolojia.
Alieleza
kuwa ukuaji wa kisekta umepelekea kuundwa kwa mamlaka ya mawasiliano
kwa lengo la kuratibu mawasiliano ndani ya jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania isipokuwa Sekta ya utangazaji kwa Upande wa Zanzibar kwa vile
tayari ina Tume yake ya Utangazaji.
Profesa
Mbarawa alifahamisha kwamba Mtambo huo maalum wa usimamizi wa masafa
ya mawasiliano Zanzibar uliogharimu shilingi Milioni mia saba na
hamsini za Kitanzania { 750,000,000/- } utasaidia kuviweka salama
vyombo vya usafiri Angani na Baharini Nchini.





0 comments:
Post a Comment