Mtalamu
wa mambo ya Habari kutoka Smole Bw. Ali Rashid Salim akifahamisha kitu
katika mafunzo ya wandishi wa Habari juu usajili wa Ardhi,katika ukumbi
wa Wizara ya Habari kikwajuni Mjini Unguja jana.
Afisa
mtambuzi wa Ardhi Unguja Shawana Soud Khamis akitoa elimu ya Utambuzi,
kuisajili na kuitumia Ardhi kwa wandishi Habari katika ukumbi wa Wizara
ya Habari kikwajuni Mjini Unguja jana.
Baadhi
ya wandishi Habari wa vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa makini mafunzo
yanayotolewa na Mtalamu wa mambo ya Habari kutoka Smole Bw. Ali Rashid
Salim (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Habari kikwajuni Mjini
Unguja jana. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
======== ======= =======
Maryam Fumu na Patima Mtumwa Maelezo- Zanzibar.
Afisa
Mkaguzi wa Ardhi Zanzibar Shawana Suod Khamis amewataka wananchi kutoa
mashirikiano katika kufanikisha zoezi zima la Utambuzi na usajili wa
ardhi nchini.
Kauli
hiyo imetolewa jana katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utamaduni na
Michezo wakati akifunga mafunzo ya siku moja ya utambuzi na usajili wa
ardhi kwa waandishi wa habari .
Alisema
kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuweza kuwapa mbinu za kisasa na
uwelewa mpana kwa waandishi ili kuweza kuihamasisha jamii kuhusiana na
zoezi hilo.
Alieleza
kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya
Finland kupitia mradi wa SMOLE II unaendelea na zoezi la usajili wa
Ardhi kupitia maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
Shawana
ameyataja baadhi ya maeneo ambayo tayari yameanza zoezi hilo na
kuonyesha mafanikio kuwa ni Kijiji cha Nugwi , Jendele, Paje,
Chwaka, Kwaalinatu ,Mji Mkongwe, Mkokotoni ,Mwembetanga , Rahaleo,
Muembeladu, Muembeshauri, Gulion, Kibondeni, Kisima Majongoo,
Mchangani na Vikokotoni .
Akieleza
baadhi ya faida za usajili wa ardhi kuwa ni kupunguza migogoro
inayotokea mara kwa mara katika jamii na kumsaidia mmiliki wa ardhi
katika kupata mikopo katika benki, mashirika na taasisi mbali mbali.
Mkufunzi
wa mafunzo hayo Afisa Habari na Mawasiliano wa SMOLE Ali Rashid Salim
amesema migogoro mingi ya Ardhi husababisha usheleweshaji wa mirathi
kwa jimii hasa kwa wanawake watoto yatima na watu wenye ulemavu na
kupelekea kukosekana kwa haki kwa wahusika.
Zoezi
la usajili wa ardhi limeanza rasmi mwaka 2008 inatarajiwa kuwa
ifikapo mwaka 2015 asilimia 50 ya ardhi yote ya Zanzibar iwe tayari
imeshasajiliwa .
0 comments:
Post a Comment