Waziri
wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee, na Balozi Mdogo wa China Zanzibar,
Xie Yun Liang, wakitiliana saini msaada wa dola milioni 6. (Picha na
Maktaba).
Na Ali Issa na Mariam Fumu Maelezo-Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini mkataba wa makubaliano na
Serikali ya China ambapo nchi hiyo itaipatia Zanzibar msaada wa zaidi
ya Dola milioni sita za Marekani ikiwa ni uendelezaji wa misaada
inayotolewa na nchi hiyo kwa Zanzibar katika nyanja mbali mbali za
Uchumi.
Sherehe
za utiaji saini makubaliano hayo zilifanyika katika Wizara ya Fedha,
Vuga ambapo Waziri wa Wizara hiyo Omar Yussuf Mzee aliiwakilisha
Zanzibar na Balozi mdogo wa China hapa Zanzibar Xie Yunliang
aliiwakilisha nchi yake.
Akizungumza
baada ya utiaji saini, Waziri wa Fedha alisema kua msaada huo utalenga
katika nyanja mbali mbali ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee
Mkoani, Uchimbaji wa visima vya maji safi na salama na kupambana na mbu
wa malaria katika maeneo ambayo maradhi hayo bado yapo.
Alisema
kazi iliobakia hivi sasa ni kwa Idara ya Hazina kuwasiliana na
wahusika ili utekelezaji wa makusudio hayo yaweze kufikiwa kwa haraka.
Nae
Balozi Xie Yunliang alisema kuwa Zanzibar na China ni nchi mbili zenye
uhusiano mzuri wa muda mrefu hali ambayo imeifanya kua ni rafiki wa
karibu.
Alisema
makubaliano hayo ni muendelezo wa misaada wanayoitowa ili kuona
Zanzibar inapiga hatua katika juhudi zake za kukuza Uchumi na Maendeleo
ya wananchi.
Utiaji
saini makubaliano hayo ulikwenda sambamba na kukabidhiwa hati za Taa
za Barabarani zinazo tumia nishati ya jua katika Manispaa ya Mji wa
Zanzibar ambapo mradi huo ulifadhiliwa na Serikali ya China.
0 comments:
Post a Comment